SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kumi na Tisa (19)
"Naam. Dawa ya mzizi tayari sina mwilini,dawa ambayo ingenifanya nipotee katika mazingira yoyote. Sasa nimebaki na hirizi,hii ni dawa ambayo itanipatia nguvu nyingi katika mwili wangu. Laiti kama ile dawa ningekuwa nayo,basi nisingetumikia jela mimi.
Mimi ni Zabroni, hata hivyo sitokubali. Kupitia hirizi hii hii nitatoroka humu nikalipe kisasi,kamwe mwanamke hawezi kushindana na mimi. Kamwaga mboga acha mimi nikamwage ugari", yalikuwa ni mawazo ambayo Zabroni alikuwa akiyafikiria ndani ya kichwa chake, muda huo akiwa amelala usiku na wafungwa wenzake.
Kesho yake palipo pambazuka,Zabroni alikuwa mtu wa kwanza kuamka kabla hata kengere haijagongwa. Bluyner alikuwa mtu wa pili kuamka,ambapo alishangaa sana kumuona Zabroni kadamka sana kuliko siku zote tangu aanze kutumikia kifungo chake cha maisha jela. Bluyner aliachia tabasamu la kebehi kisha akasema "Naona leo umekuwa mtoto mtiifu,bila shaka shauri ya kipigo ndio imekufanya leo uwe mtiifu",alicheka kidogo halafu akaendelea kusema "Kwa muendelezo huu utafaa kuwa mke wangu kwani mimi napenda sana mwanamke mtiifu hasa kama wewe,sawa?..",alisema Bluyner akimdhihaki Zabroni ilihali wakati huo Zabroni aliishia kumtazama bila kujibu chochote.
Bluyner baada kuona Zabroni yupo kimya alizipiga hatua kumsogelea ,alipo mfikia aliusogeza uso wake jirani kabisa na uso Zabroni kisha akambusu. Kitendo ambacho kilimkera Zabroni,alipandwa na hasira moyoni mwake. Alikunja ngumi nzito Kwenye mkono ule aliovaa hirizi kwa nia ya kumpiga Bluyner. Lakini kabla hajairusha ngumi yake,ghafla alishikwa mkono.
Hapo aligeuka nyuma akamtazama aliyemshika mkono, ni moja ya wafungwa wenzake mule gerezani anaitwa Steve swahiba wake sana Zabroni gerezani. "Zabroni braza, na braza Bluyner. Tunafahamu fika nyie ni miamba ndani ya hii jela,ingawa Zabroni bado hujaonyesha umwamba wako lakini simulizi fupi ya maisha yako inajidhihirisha kuwa wewe ni mwamba.
Aamh Kaka Bluyner. Wewe ni mwamba pia,kila mmoja ndani ya hili gereza anafahamu kimbembe chako. Hivyo basi haina maana kutunushiana misuri asubuhi yote hii,heri mpange siku moja mkutane ndipo muanze kuonyoshena umwamba",alisema Steve huku akiwaamulia vijana hao ili wasipigane.
Ukweli ni kwamba Zabroni safari hii alipania avunje ukimya lakini baaada kupewa maneno hayo na swahiba wake aliona bora atulize hasira zake ili siku moja amuadabishe mbele ya wafungwa wenzake.
Na mara baada Steve kuwaamulia wanaume hao,punde si punde kengere ya kuawamsha wafungwa iligongwa. Ndipo wafungwa wote walipotoka vyumbani haraka sana wakawahi mstarini kuhesabu namba.
Amabapo zoezi hilo lilichukua dakika kadhaa likawa limekamilika,hatimaye walipewa uji waakanywa kwa muda mfupi sana wakawaa wamemaliza. Shughuli ikawa imebaki kwenda shambani kulitumikia taifa kwa nguvu bila kubembeleza,maisha ambayo kijana Zabroni aliyachukia sana kiasi kwamba roho ilimuuma ilihali hasira zake nyingi akiashumu ni kitendo gani atakacho mfanyia Veronica ikiwa kama njia sahihi ya kulipa kisasi juu ya kile alicho mfanyia.
"Acha kuzubaaa panda gari twende kenge wewe",ilikuwa ni sauti kutoka moja ya Askari magereza aliyekuwa akimwambia Zabroni ambaye alionekana kusweta na usongo wa mawazo. Zabroni aligeuka kumtazama huyo Askari aliyemwambia hayo maneno kisha akarudisha uso wake kunako gari lile lililosheni wafungwa,akapanda safari ikawa imeanza.
Upande wa pili,Bruno ama Mr Rasi alikuwa mtaani akitembea tembea hana hili wala lile. Hatimaye alikatiza moja ya mitaa ambapo huko alikutana na kundi la watu wakifanya dili haramu,dili hilo lilikuwa la mapigano.
Umati wa watu ulikusanyika mahali hapo wakishangaa ngumi hizo huku pembeni napo vikionekana viti wakiwa wamevikalia vibopa ama kwa lugha nyepesi unaweza kusema matajiri.
Ngumi zililindima ,shangwe zililipuka kutoka kwa watazamaji. Na mwisho wa pambano ilisikika sauti ikisema "Vipi Bwana Karani,unamwingine tena?..",sauti hiyo ilisikika kutoka kwa mmoja wa bosi aliyekuwa mahali hapo akipambanisha watu wake na watu wa bosi mwingine,hiyo ikiwa kama njia ya kusaka pesa. Bosi huyo aliitwa Derick.
Karani alishusha pumzi kisha akajibu "Sina,ila siku zote usikariri maisha. Sio kila kobe akiinama basi anatunga sheria,hapana kombe wengine wanawaza akupe hukumu gani?.."
"Hahahahaah",alicheka Derick baada kusikia msamiati wa Karani,baada ya kicheko akajibu "Sawa sawa. Lakini epukana na zogo za ubunuasi kaka,tukutane SOPHIE HOTELI unipatie pesa zangu. Ukiitaji ligi tena mimi nipo tayali " alisema Derick. Mr Rasi,yote hayo aliyasikia.
Hivyo aliona hapo ni mahala pakupiga pesa lakini pia ni sehemu sahihi pakujificha ili mkono wa dola usimfikie akiamini kwamba matajiri hao mpaka wanaamua kuanzisha biashara hiyo haramu basi lazima kutakuwa na kitu wao na serikali.
"Nijikosheje mbele yao? ",alijiuliza Mr Rasi wakati huo watu walionekana kusambaa baada ya mpambano kumalizika. Kabla hajapata jibu,mara ghafla kundi la vijana wasio pungua saba walimzunguka. Mr Rasi alistuka kuwekwa kati wakati huo huo kijana mmoja kati ya wale sababa akimwambia "oya! Unaonekana mgeni sana haya maeneo.
Naomba utuambie umefuata nini sehemu hii?..". Mr Rasi hakumjibu. Kitendo ambacho kilimkera sana yule kijana ambapo alirudia kuhoji kwa sauti ya juu "Umefuata nini?..",bado Mr Rasi hakujibu. Hapo ndipo yule kijana alipowaamuru vijana wenzake sita wampige Mr Rasi.
Ndani ya nafsi yake Bruno akasema "Naam! Ama kweli mwanaume siku zote halali na njaa ila atachelewa kula. Acha niwaonyeshe" ,kichapo kiltembezwa hapo. Tajiri Derick hakushuhudia ule mpambano ila tajiri Karani aliushuhudia namna Mr Rasi alivyokuwa akiwapa dozi wale vijana waliojifanya watoto wa mjini.
"Bosi huyu jamaa hutakiwi kumuacha",alisema mmoja wa mpambanaji wa Karani. Karani hakujibu,aliendelea kumtazama Mr Rasi huku akitabasamu. Moyoni akajisemea "Yes kijana mtamu sana huyu ananifaa kivyovyote vile.
Ahahahaaa Derick umekwishaa " ,alimaliza kwa kicheko Karani,ilihali upande wa pili umati wa watu kutoka maeneo mbali mbali walikusanyika kuja kushangaa huo ugomvi,kwa maana wale walinzi waliokuwa wakilinda pembeni kuwazuia baadhi ya watu,nao waliondoka baada kusikia kwamba kuna mpambanaji anapigana na watu sita mmoja wa nyogeza.
Jumla watu saba. Hivyo kitendo kile cha kuachia muanya kiliwafanya watu kuja kwa wingi sana kushuhudia hilo pambano la Mr Rasi na hao wahuni wa mjini.
Ndani ya watu hao waliokuja kutazama mpambano alikuwemo na Tina,safari hiyo Tina alikuwa na shangazi yake. Tina alifurahi sana kumuona Mr Rasi kwa mara nyingine tena. Aliachia tabasamu pana huku pole pole moyo na nafsi yake ikionyesha kuvutiwa na mtu huyo. Mr Rasi ama Bruno adui yake Zabroni,wakati huo huo Zabroni na Tina ni wapenzi.
Kwingineko baada ya shuguli kumalizika, wafungwa walitulia kwanza kabla hawajapanda kwenye magari yao ili kurudishwa gerezani. Nafasi hiyo sasa Bluyner aliitumia kumchoza Zabroni ili wapigane,baada ya pambano kila mmoja ajulikane nani mwamba.
Bluyner alimuita mmfungwa mmoja kisha akamtuma kwa Zabroni. "Sikia, nenda kamwambie Zabroni kuwa mumewe namuita". Upesi mfungwa huyo alimfikishia ujumbe Zabroni kama ulivyo, Zabroni akajua fika kuwa tayari Bluyner anahitaji pambano,Kwahiyo kwa kuwa hirizi anayo akaona hakuna haja ya kuogopa.
Hivyo naye alimtuma mfungwa mwingine akamwambia "Kwambie Bluyner Zabroni kasema ipo siku atakulawiti",Tusi hilo lilipomfikia Bluyner alikasirika, hima akamfuata Zabroni kwa niaba ya kupigana. Zabroni kwa sauti akasema "Sikilizeni hakuna kuingilia kati", maneno hayo Zabroni aliyasema kwa hasira huku akiwa tayari kupigana huku akiwa na nia moja tu mara baada ya pambano hilo asirudi Gerezani. Moja kwa moja atoroke akalipe kisasi kwa Veronica pia akamalizane na Bruno. Mr Rasi.
Baada Zabroni kuwataka wafungwa wenzake wasiamulie ule ugomvi,upande wa pili nako Askari waliokuwa wakiwasimamia waliambizana kwamba waache waone nani mbabe. Hivyo walijifanya wako bize kupiga zogo ilihari huku wafungwa tayari wameshaweka uzio kwa duara ili kuangalia mpambano. Mtu wa kwanza kurusha ngumi alikuwa Bluyner, alirusha kumi na mateke harakaraka yaliyomfanya Zabroni kurudi nyuma akiyakwepa mateke hayo.
Lakini licha ya kurudi nyuma ila teke moja lilimpata,Zabroni akawa ameanguka chini. Nafasi hiyo Bluyner akaitumia kujirusha juu mfano wa sama soti kisha akatua moja kwa moja kwenye kifua cha Zabroni. Zabro alitema mate ya damu,wafuasi wake wakashika vichwa vyao ilihari upande wa wafuasi wa Bluyner wao walilipuka shangwe huku wakimtaja Bluyner kwa kumshangilia.
Upande mwingine yule Askari aliyempatia Zabroni hirizi alionekana kusikitika pia kuingia na hofu,alihofia uwezo wa Zabroni kupigana Bluyner kijana ambaye alionyesha uwezo wa juu kupigana.
"Amka sasa nikunyooshe! Amka sasa kama unayaweza",alisema Bluyner huku akipiga kifua chake. Zabroni aliweka mikono yake kifuani kudhihirisha kwamba kaumia eneo la kifua. Baada ya hapo alinyanyuka kisha akasimama ila kabla hajakaa sawa,Bluyner aliruka juu kwa mara nyingine akiwa angani alirusha mguu wa kulia juu ya kichwa cha Zabroni, na mguu wa kushoto ukawa umempata ambapo Zabroni alianguka chini kama mzigo kisha akaanza kupumua kwa shida. Pigo mbaya sana hilo alilopigwa kichwani kiasi kwamba alihisi Malaika mtoa roho anamnyemelea. Wakati huo huo Bluyner alimsogelea akachuchumaa chini akamtazama usoni,akacheka kisha akasema "Zabroni, wewe huna uwezo wa kupigana na mimi.
Amini kwamba walionichangua kuwaongoza nyinyi abadai hawakukosea,sasa iweje uthubutu kuangusha mwamba ulio shindikanika?", akacheka Bluyner kwa mara nyingine tena halafu akaendelea kusema "Umepima maji kwa kijiti pasipo kujua kuwa mahali hapa kuna kina kirefu,kwanini usizame? ", kwisha kusema hivyo alirudia tena kucheka kisha akakunja ngumi kwa niaba ya kumpiga Zabro lakini kabla hajaishusha ngumi,Steve alifika haraka sana akamshika mkono ule uliokuwa umekunja ngumi.
Wakati huo upande wa pili Askari waliokuwa na jukumu la kuwarinda na kuwasimamia hao wafungwa,wao walikuwa kando wakishuhudia huo mpambano. Askari mmoja kati yao alipotataka kuingilia kati alizuiwa na yule Askari aliyemrudishia Zabroni hirizi. Hivyo ikabidi watulie waangalie nani bingwa ingawa Askari huyo aliyempa hirizi Zabroni, moyoni hakuwa na amani kama Zabroni ataweza kuibuka kidedea.
"Bluyner, tafadhali naomba umuache. Tayari umejizihirusha kuwa wewe ni nwamba. Naomba usiendelee kumpiga utamuuwa kaka nielewe tafadhali", alisikika akisema hivyo Steve huku akiwa ameung'ang'ania mkono wa Bluyner uliokunja ngumi.
Bluyner alifura hasira mara dufu ambapo alinyanyuka kisha akamtazama Steve usoni,Steve aliogopa lakini hakusita kumuombea msamaha rafiki yake kipenzi. Bado aliendelea kumuombea msamaha Zabroni,kitendo ambacho kilipelekea kipigo kuhamia kwake.
Alipigwa sana Steve wakati huo Zabroni pale alipokuwa amelala ghafla kumbukumbu ilimjia, ambapo alikumbuka maisha ya nyuma kidogo kabla ile dawa iliyomfanya asumbue kila mahali haijapotea mwilini. "Mimi ni Zabroni! Mimi ni Zabroni",nisauti ambayo ilikuwa ikijirudia kichwani mwake wakati huo akikumbuka baadhi ya matukio aliyowahi kufanya.
Alikumbuka jinsi alivyomtumbua mama mjamzito, alikumbuka ugomvi mkubwa aliowahi kupigana na Madebe pia Bruno ambaye kwa sasa Mr Rasi. Yote hayo ikiwa ni ndani ya kulipa kisasi cha wazazi wake ingawa marehemu Madebe na Mr Rasi waliingilia ugomvi huo ukiwa hauwahusu.
Basi kumbukumbu za Zabroni hazikuishia kwenye matukio hayo tu lahasha alikumbuka zaidi mpaka alivyozama kwenye penzi la Afande Veronica pasipo kutambua kwamba Veronica ni Afande na yupo kwa niaba ya kumtia katika mikono ya sheria,jambo ambalo lilikwenda sawai.
Hapo sasa ndipo Zabroni alipotikisa mkono,mara ghafla akahisi kumuona mtu aliyevaa nguo nyeupe akimsogelea mahala pale alipoangukia baada kupokea kichapo kikali kutoka kwa Bluyner. Mtu huyo aliyevaa nguo nyeupe alikuwa akimfuata Zabroni huku akisema "Amka Zabroni, wewe ni mwanaume hupaswi kushindwa kizembe. Aaamka Zabroni amka babaaa ",sauti hiyo baada kulindima ipasavyo kichwani mwa Zabrini, hatimaye alijihisi kupata nguvu.
Alifumbua macho yake kisha akasimama,ilihari upande mwingine kijana Steve alikuwa akichezea kichapo huku baadhi ya wafungwa wakiingilia kati kumtetea ambapo baada kuonekana bado Bluyner anakuwa mgumu kumuachia,Askari nao waliingilia kati lakini Bluyner alizidi kumganda Steve akigoma kumuachia. Hivyo hapo pakawa hapatoshi,vurumai la kutisha lilizuka sehemu hiyo ila lilikuja kutulia baada kusikika sauti ya Zabroni ikisema "Mimi ni Zabroni! ",wafungwa wote akiwemo na Bluyner waligeuka kutazama kule ilipotokea sauti hiyo.
Walimuona Zabroni akiwa amesimama kidete huku mkono wake wa kulia wenye hirizi akiwa amekunja ngumi moja nzito ikiwa uso wake nao ukisweta jasho mchanganyiko na damu. Wafungwa baadhi walio mkubali Zabroni walishangilia baada kuona kidume kanyanyuka. Bluyner alizungusha shingo kuilaza kulia na kushoto,mishipa ililia mfano wa kijiti kilicho vunjika kisha akamsogelea Zabroni huku akiwa ametunisha mbavu zake.
INAENDELEA