KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu YaSaba (07)

simulizi ya penzi la mfungwa

"Kijana yule tuliyepisha naye juzi jioni wakati ulipokuja kunipokea", mwemyekiti alivuta kumbukumbu kwa muda wa sekunde kadhaa mwishowe akakumbuka kuwa mtu mwenyewe ni Zabroni mtoto wa mzee Ndalo. "Sawa nitazijuaje hizo nyayo?..", kwa mara nyingine tena aliuliza Mwenyekiti. 

Mzee Baluguza alikaa kimya kidogo huku akichukuwa kipande cha kitambaa ambacho kilionekana cheusi kisha akamkabidhi Mwenyekiti halafu akamwambia "Kavaa saganyoka,hivyo ni rahisi sana kuzigundua. Nenda haraka chukua mchanga kudogo hapo alipo kanyaga kisha niletee hapa nimalize kazi", alijibu mzee Baluguza. Mwenyekiti akiwa na wasiwasi kwa kijana Zabroni alifanya kama alivyo ambiwa kisha haraka sana akarudi wakati huo mzee Fungafunga akiwa kama mmoja ya baraza la wazee kwenye mkutano huo yeye alikuwa akiwaongelesha huku mzee Baluguza akifanya yake. 

Mara baada kumaliza ndipo huyo mzee alipo simama na kisha kusema "Habari zenu wanakijiji, jina langu naitwa Baluguza nadhani wapo wanaonifahamu na wasio nifahamu. 

Nimekuja hapa kutokomeza hili janga linalo endelea hapa katika kijiji chenu. Haya mauwaji yakinyama, yanatisha lakini leo ndio siku kuu ambayo mtu huyu mshenzi na mjinga atagundurika. ", aliongea kwa kujiamini kabisa Baluguza punde akaendelea kusema." Rafiki yako ndio huyo huyo adui yako, kwa maana hiyo basi kikulacho kinguoni mwako. 

Mtu anayefanya vitendo hivi wala hatoki nje ya kijiji hiki ila mpo naye humu humu" alisema Baluguza, akameza mate halafu akaendelea kusema. 

"Kwa maana hiyo basi leo lazima agundulike huyu mtu anaye uwa watu wasiokuwa na hatia, na akishagundulika ndipo kijiji kitaamua mtu huyu afanywe kitu gani. Je, mpo tayari?.." Sauti za wanakijiji zilipasa zikisema "Tupo tayariiiiii!" 

Lakini wakati wanakijiji hao wanapasa sauti zao kutaka kumfahamu kirusi wa kijiji mara ghafla ule moto uliokuwa ukitambaa kwenye kamba hatimae ilifika kwenye nyumba,nyumba ya mzee Ngurumo ikaanza kuteketea ikiwa mchomaji yupo hapo hapo kwenye mkutano wakati huo mzee Baluguza akitaraji kumuumbua mchomaji huyo mbele ya wanakijiji.

Moto ule uliokuwa unawaka kwenye nyumba ya mzee Ngurumo uliwastua sana wanakijiji,pia hata mzee Baluguza naye alionyesha kustuka ingawa sio rahisi kutumbua endapo kama ukimtazama usoni kwa pupa. 

Ngurumo alitaharuki baada kuona nyumba inaungua, alipasa mayowe huku akijing'atua eneo alilokuwa amekaa akitaka kwenda walau kuokoa baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani,lakini kabla hajaondoka,Mwenyekiti alimshika mkono akamvuta karibu yake kisha akasema "Hata ukiondoka hutaweza kuokoa kitu chochote mzee mwenzangu, kwahiyo nakusihi hebu punguza jazba ili leo tumtambue kirusi wa kijiji hiki" alisema Mwenyekiti akimwambia mzee Ngurumo ambaye muda huo alikuwa akilia kilio cha mtu mzima. 

Mke wake alisimama akilia machozi mithili ya mke aliyefiwa na mumewe,mwanamke huyo akamkumbatia mumewe huku akiangua kilio. Kitendo hicho kilitia simanzi mkutanoni hapo,baadhi ya wakina mama na wakina baba wenye hekima walijaribu kuwatuliza wazee hao,nao kila mmoja alitulia kwa muda wake ingawa mioyoni mwao wakiwa wamefura hasira zisizo na mfano.

Utulivu ulipo tawala,mzee Baluguza akaanza kufanya mambo yake akiwa na nia ya kumuweka hadharani kirusi huyo wa kijiji,kwenye mti mnene kiasi alibandika kitambaa cheupe huku akiimba nyimbo zake za asiri. 

Alipo maliza aliwaambia wanakijiji wawe makini kukitazama hicho kitambaa umakini na utulivu ukaongezeka kwa wanakijiji hao ilihali kijana Zabroni naye akiwa hajui chochote ila aliamini kuwa huyo mzee hawezi kitu chochote juu yake. Na wakati akijiaminisha hayo ndani ya nafsi yake,Ghafla kwenye kile kitambaa cheupe alionekana Zabroni akiwa anafanya kile kitendo kwenye Nyumba ya mzee Ngurumo. Wanakijiji walitaharuki kila mmoja alionekana kushungaa, ilihari Zabroni naye alijikuta akijishangaa na kujiuliza maswali mengi kichwani mwake juu ya kile kilicho kuwa kikiendelea kwenye kitambaa kile cheupe. 

Aliingiwa na hofu pasipo kuchelewa alisimama akaanza kunuia maneno yake ili apate kupotea maeneo hayo lakini kabla hajatamka chochote,kundi la wanakijij likaanza kumvagaa na kisha kumpiga. Zabroni alichezea kipigo cha mbwa mwizi ila baadaye kidogo alifanikiwa kupotea katikati ya umati wa watu,ajabu aliwaachia nguo zake tu. 

Kitendo hicho kiliwastua wanakijiji,hapo sasa kila mmoja akajawa na hofu huku maswali yaliyokosa majibu yakitawala akili mwao. Ni kitendo ambacho kilimshangaza sana mzee Baluguza, alijiuliza uwezo gani alio nao kijana huyo, Na baada kumaliza shughuli hiyo aliona hakuna haja ya kuendelea kukaa kijijini hapo kwani kwa maono yake aliona kamwe hatoweza kufua DAFU kumkabili Zabroni, ili kulinda uhai wake aliamua kufunga safari usiku wa manane kurudi kijijini kwao. 

"Nayapenda maisha yangu", alijisemea mzee Baluguza ndani ya nafsi yake huku akiandaa vilago vyake. 

Hatimaye kila kitu kilikaa sawa, na sasa alianza safari wakati anatoka nyumbani hapo kwa Mwenyekiti alipokuwa amefikia,punde si punde Zabroni alitua maeneo hayo. Akiwa na lengo moja tu ambalo ni kutekeleza ahadi yake aliyojiwekea. Pasipo kupoteza muda Zabroni alichukuwa kamba yake akaitambalika kisha akachoma moto. Moto ambao ulianza kutembea pole pole kuelekea kwenye nyumba wakati huo yeye tayari ameshapotea eneo hilo,nia kuu ya kijana Zabroni kuwahi kuchoma moto nyumba ya Mwenyekiti ni kumuuwa mzee Baluguza ili apate kufanya kazi yake kwa uhuru zaidi bila kubuguziwa na mtu yoyote, aliona kama mzee huyo anataka kuharibu mkakati wake.

"Kufa tu hakuna namna mwanaharamu mkubwa wewe", aliongea Zabroni na hata asijue kuwa tayari amechelewa kwani mzee Baluguza alishafungasha vilango vyake na kuondoka zake. 

Ule moto uliendelea kutembea kwenye kamba ile kwa kasi ya ajabu ila kabla haujanasa kwenye nyasi za nyumba,zilisikika kelele za mbwa wakibweka kwa nguvu kiasi kwamba mkewe Mwenyekikiti ilimfanya aamke na kisha kumwamsha mumewe ili atoke nje akatazame ni nini kinacho endelea huko. Kumbe wakati Zabroni anaondoka nyumbani hapo kwa Mwenyekiti alijibadilisha akawa katika umbo la kutisha liliacha harufu mbaya ambayo iliwafanya mbwa kubweka kuashiria nje kuna kitu cha hatari, Mwenyekiti akamsikiliza mkewe haraka sana akatoka nje ambapo alizunguka nyuma ya nyumba akakuta moto tayari umeshika nyumba. 

"MOto moto motoooo" alilalama Mwenyekiti usiku ule wa manane, mkewe akiwa ndani akastuka alipotaka kukimbia akajikuta anazima kibatali kilichokuwa kinawaka.

Hapo sasa aliukosa mlango wa kutokea kwamaana ndani palikuwa na giza nene,upande wa pili napo Mwenyekiti alikuwa akihaha japo kuuzima kwa mchanga lakini alipoona moto unazidi kukolea alirudi hima upande ulipo mlango ili amuamshe mzee Baluguza pia amtoe ndani mke wake,lakini kabla hajafanya jambo lolote,moto ulifunika nyumba nzima kwani muda ule kulikuwa na upepo mkali uliofanya moto kutambaa kwa kasi zaidi. 

Mwenyekiti akajikuta anashindwa afanye nini, alibaki amesimama huku mikono akiwa ameweka kichwani pia akilia kilio cha mtu mzima akilitaja jina la mkewe aliyepoteza maisha kwa ajari hiyo ya moto. Baada ya lisaalimoja mwanakijiji mmoja mmoja alijitokeza kwa Mwenyekiti kuja kushuhudia kitu gani kimetokea,walimkuta Mwenyekiti wao akiwa mnyonge asijue cha kuwaambia. 

Hakika walichoka sana kila moja aliona hakuna haja ya kuendelea kuishi katika hicho kijiji cha mauaji ya kinyama,na hivyo baadhi za familia zilianza kufanya mikakati ya kukikimbia kijiji hicho.

Alfajiri mapema mbiyu ililia kwa mara nyingine,mbiyu hiyo ilitangaza maafa yalitokea kwa Mwenyekiti huku mtoa taarifa aliwajuza wanakijiji kuwa Mwenyekiti kafiwa na mke wake usiku wa jana,alienda mbali zaidi na kusema si mke wake bali na mzee Baluguza. 

Hapo wanakijiji walizidi kuchanganyikiwa kwa taarifa ile "Mmh sio bure huyu mtu atakuwa anakisasi na kijiji hiki ", alisema mzee mmoja mlemavu akiwa ndani ya nyumba yake ya matete asubuhi hiyo baada kusikia hiyo taarifa. Na wakati mpiga mbiyu anaendelea kutangaza taarifa hapo kijiji,mara ghafla akafika eneo lile walilo fanyia mkutano siku iliyopita. 

Punde alistua mpiga mbiyu huyo baada kuona damu chini ya mti huo ambao waliutumia kumwona mtukutu Zabroni akichoma nyumba ya mzee Ngurumo. 

Mpiga mbiyu akajiuliza "Damu hii kakamatwa nguruwe pori ama?..", akiwa na wasi wasi alijiuliza hilo swali,tonya la damu likamdondokea kutoka juu ya mti huo. Aliinua uso wake kutazama juu akauona mwili wa mzee Baluguza ukiwa unaning'inia huku damu zikivujia kwenye shingo. 

Alichinjwa kikatiri mtaalamu Baluguza. Mpiga mbiyu alistuka,mwili ulimsisimka huku akitetemeka kwa hofu, muda huo huo ilisikika sauti ikijirudia mara mbili mbili, ilikuwa sauti ya Zabroni Sauti ya ilisema "Zabroni! Zabroni " sauti hiyo ilimaliza kwa kicheko kizito.

INAENDELEA

Powered by Blogger.