KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mama vannessa sehemu ya kumi na saba (17)

Hadithi nzuri ya kusimumua ya mapenzi ya mama vannessa
“Pole sana najua unaumia lakini ngoja nikuulize kitu, kwenye maisha wewe unataka nini hasa?

“Furaha amani upendo na maisha bora”

“Unahisi siwezi kukupa vyote hivyo”

“Sina uhakika”

“Ok mimi nitakupa chochote utakacho na ata ukitaka aniwe mke wake itakuwa sema nini unahitaji ambacho ndicho hofu yako kubwa?”

“Familia, mimi ni kijana ambaye umri umeenda nilivyooa nilitarajia yule mwanaume anizaliwe mtoto na mimi niitwe baba.

“Jambo rahisi sana mimi nipo tayari kuuzalia mtoto ila kwa sharti moja?

“Kunizalia mtoto!!! Sharti gani hilo?

“Kwamba tutafanya siri na tutammbambikizia hiyo mimba baba Vanesa. Alafu baadaye mtoto akishakuwa ndo utamchukua.

“Mmmm sikuwahi kuwaza kama unaweza kuwa tayari kwa kila jambo. Lakini mama Vanesa kwanini unataka kunifanyia yote haya?

“Kwa sababu nakupenda”.

Lucas ilibidi awe mpole alishindwa kuelewa huyo mwanamke kwa nini aliamua kujitoa muhanga kiasi hicho. Hakuelewa na haukamini kama mke wa boss wake anaweza kumkubali kiasi hicho na eti yupo tayari hata kumzalia mtoto.

“Mama Vanessa nahisi hujui ulisemalo. Nahisi wewe umachanganyikiwa na ndio maana unaongea vitu ambavyo hutoweza kuzifanya. Yaani wewe kila kitu unataka kunifanyia.. Nikuombe nikupe muda ukatafari kila jambo tulilotenda na yulilopanga kutenda na ni madhara yake.. Ukishatafakari ndo tuje tuzungumze tena hata mimi nahitaji tafakari kidogo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Asante Luas usiwe na hofu maihsa ni mipango na kwa kuwa unaonekana uniamini nipe huo muda unaousema nitakuaminisha. Kwa sasa mimi narudi zangu Musoma tutazidi kuwasiliana na utanitafuta kwa namba ile ya siri ambayo nimeinunua kwa ajali yako tu.

“Sawa haina shida safari njema.”

Walaigana kwa mtindo huo na mama Vanesa aliondoka na safari ya kurudi Musoma ilianza. Alipanga kushukia Bunda ili kufuatilia mambo yake ya biashara na akifika huko ndo ampigie mumewe. Alifika Bunda baada ya masaa mawili. Alifika kwenye moja ya sehemu yao ya biashara. Hapo alipigwa na butwaa mara baada ya kumkuta mme wake. Alipanga kumdanganya kuwa alikuwa huko..
Alirudi kinyumenyume na kuamua kuondoka zake. Mishale ya hatari ilipiga kichwani mwake na kuhisi kama wataonana huko inaweza kuleta shida. Alihisi kuwa ataulizwa maswali ambayo kwa kweli atashindwa kuyajibu na kufanya mambo kuzidi kuwa magumu. Alirudi kisha kupanda gari na kuanza safari ya kwenda Musoma. Baada ya kupanda gari aliamua kuwasha simu ili kuona sms zilizoingia na jinsi ya kujipanga kama atakuta za mme wake. Akiwa njiani kuna sms iliingia kupitia namba ngeni.

“Najua hunijui lakini mimi nakujua. Kama mwanamke mwenzangu hili linaniuma sana maana si kwa umalaya huu. Ni hivi mumeo yupo Bunda na anauhusiano wakimapenzi na binamu yako Lisa yule ambaye anasimamia biashara zenu huku Bunda. Ingia WhatasApp nimekutumia ushaihidi wa picha usije sema nataka kuivunja ndoa yako.” Ilikuwa ni sms iliyotumwa na mtu ambaye hakujitambulisha ni nani. Mama Vannesa alirudia kuisoma ile sms zaidi ya mara tatu kisha akawasha data ili kuona hizo picha. Ni kweli mme wake alikuwa yupo na ndugu yake huyo. “Jamani Lisa mbona ataniua kwa presha” mama vanesaa aliropoka mara baada ya kuona moja ya pozi ambalo lilionesha kuwa kuna kitu kilikuwa kikiendelea. Machozi yalimlengalenga na alijuta kuolewa na mwanaume huyo. Roho ilimuuma sana na alishindwa kuelewa baba Vanesa alikuwa na pepo gani.

Ingawa picha hizo hazikuonesha moja kwa moja kuwa kulikuwa na ushaidi kuwa watu hao ni wapenzi lakini kilichomuuma ni binamu yake kumdharaua. Anakumbuka alishamuonya kuwa kamwe hasiweke mazoea na shemeji yake lakini yeye amaemua kumgeuka. Atakipata anachokitafuta na kumuoneshea kuwa mimi huwa sijaribiwi safari yake ya kurudi kijijini imeiva. Nitamrudisha ndio nitamrudisha hata kama ndugu zangu watanichukia ila hawezi kuwa na uhusiano na mme wangu.” Mama Vanesa aliwaza vitu vingi sana huku akijiuliza kwa nini mambo hayo yanamtokea wakati huu. Alijiuliza pia kwanini mme wake hakumtafuta jana na kutaka kujua alilala wapi. Aliona ishara zote kuwa kwa sasa ndoa yao inakwenda kuharibika.

INAENDELEAA
Powered by Blogger.