KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mama vannessa sehemu ya kumi na sita (16)

Hadithi nzuri ya kusimumua ya mapenzi ya mama vannessa
Wote walifurahia na kuendelea kuweka mikakati huku mama Vanesa akisisitiza na anatamani raha hizo ziendelee milele katika maisha yake. Mama Vanesa aliongea kwa hisia sana na alionesha ni jinsi gani alivyokuwa amechoshwa na penzi la baba Vanessa. Hadi muda huo mama Vanesaa alikuwa hajawasha simu. Na alikuwa hataki kufanya hivyo mpaka hapo atakapofika nyumbani.Alijua kabisa ugomvi wake utakuwa mkumbwa sana.

“Kwa hiyo Lucas mimi kwa raha nilizozipata naomba tuendelee kuwa wapenzi wa siri. Kama tatizo ni pesa, hilo niachie mimi nitakusadia utafanikiwa ..Nihadi kama utaweza huu mpango.

“Nitaweza mama Vanesaa lakini mwish wa hili ni nini?”

“Utakuwa aumelipa kisasi na dawa ya kisasi ukilipe kwa muda mrefu..Tusiwe na haraka sana maana hatutafanikiwa kama baba Vanesaa akigundua kwa haraka nia yetu.

“Sawa mama Vanesa mimi nipo tayari kwa yote ila hakikisha unanisaidia kutoka kwenye hali hii ya umasikini..

“Hilo ondoa shaka kwa kuanzia …” alisita kidogo kisha kuvuta mkoba wake na kutoa hundi. Alimwandikia pesa ya kutosha ili aende kutoa banki. “Hii itakusaidia ulipe kodi na ningekushauri kama ungeweza hama Musoma..

“Kwa nini nihame Musoma?

“Kwa sababu za kiusalama maana baba Vanesa sio mtu mzuri kabisa anaweza hata kutoa uhai wako..

“Sawa basi nitahama kwa kuwa kodi yangu na yenyewe imeisha lakini….”Lucas kabla hajamaliza alikatishwa.

“Lakni nini? Sikia nakuomba usiwaze tena kuhusu ile kazi yako ambayo ulikuwa ukiifanya mwanzo. Ile itakutia matatizoni zaidi. Tena usiangaike na habari za kwenda sijui idara ya kazi ni kupoteza muda wako. Baba Vanesa ni mtu anayeheshimika sana na ni mtu muhimu sana kutokana na michango yake ingawa hayo yake ya ufirauni na uhuni huwa hayapewi uzito. Ana watu wengi sana hivyo hutoweza kumshinda.

“Mama Vanessa nakuelewa sana na nipo tayari lakini tambua roho inaniuma sana. Kwa nini anipokonye mke wangu?.Mwanamke niliyetoka naye mbali. Mwanamke ambaye nimemsomesha na kumgharamia sana.

INAENDELEA
Powered by Blogger.