KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Ni Shiida! Sehemu Ya Kumi na Mbili (12)

 LOVE STORY: ni shiidaI - 12
"Ina maana Mama Zai ndiyo alikuwa amepiga?"
"Sijui mama, wala sikuangalia jina!"

Alichokifanya mama Juliana ni kuangalia sehemu ambazo simu ile imepokelewa na kugundua kuwa alifanyiwa mchezo na Juliana. Mchezo wa kukatiwa simu ya Bitungu.
"Kwa nini umekata simu yangu!"

"Hapana mama iliita yenyewe na kukatika!"
"Ina maana miye mjinga sijui simu? si nakuuuliza?"
"Kweli mama!"

Mama Juliana aliiweka pembeni ya bafu simu ile na kumfukuza Juliana arudi chumbani aendelee na kazi ya usafi.
Juliana alijirudia zake ndani akiwa amejiongeza vya kutosha, alishaelewa picha kamili juu ya kitakachotokea mbeleni. Alichoamua ni kwenda kuchukua simu yake na kumpigia Bitungu.
"Haloo!"

"Yes baby! Nimekumisi upo wapi sasa hivi?"
"Nipo maeneo ya mbali kidogo!"
"Si uniambie tu hata kama mbali, mbali mbinguni bwana"
"Sweet niko Bagamoyo lakini kesho nategemea kurudi!"
"Bagamoyo? Umeenda lini?"

"Embu subiri kwanza kuna simu ya bosi wangu inaingia, ntakupigia."
Aliongea Bitungu kisha akamkatia simu Juliana. Juliana aliishiwa pozi, penzi la Bitungu lilishamkolea, alijifariji na kuona kuwa huenda ni kweli Bitungu atakuwa amepigiwa simu na bosi wake. Akiwa bado anatafakari kuhusu Bitungu kwa mbali akasikia sauti ya mama yake ikiongea na simu. Hatua kwa hatua akasogelea hadi eneo la sebuleni ambapo mama yake alikuwa na kanga moja tu ametoka kuoga huku akiongea na simu.

"Niambie moja nijue nikukute wapi?"
"Utakuja moja kwa moja hadi gesti ya Tupendane ipo mtaa wa Mchopanga huku Bagamoyo,"
"Kwa nini mpenzi wangu umeamua kwenda mbali huko! Embu njoo mjini bwana!"

"Hukuhuku ndiyo safi na kuna amani kuliko huko kuwa na hofu kibao, kwanza dakika 40 tu umeshafika!"
"Haya ngoja nivae haraka nakuja, nilivyo na hamu asikwambie mtu na leo nataka mechi ya kikubwa, sitaki mechi za mchangani za kuishia nusu saa."
"Kwa hilo usijali, miye ndiye Bitungu!"

"Haya mpenzi nipe saa moja nitakuwa nimeshafika hapo."
Maneno ya Mama Juliana aliyokuwa akiongea kwenye simu yalimuumiza sana Juliana, alijinyong'onyea huku akiwa bado amejificha kwa kujibanza kwenye ukuta wa sebuleni kwao, mama Juliana hakutambua kama Juliana ameyasikia yote aliyoongea kwenye simu.

Alichokifanya Juliana ni kukimbia chumbani kwake na kujiandaa tayari kwa kumfuatilia mama yake hadi atakapoelekea, lengo lake kubwa lilikuwa ni kuhakikisha anamtenganisha Bitungu na mama yake.
"Juliana!"
"Abee mama!"

"Natoka ila nitawahi kurudi mwanangu, nimeitwa sehemu kuna mwenzetu anatakiwa kufanyiwa kicheni pati hivyo nimeitwa kushirikiana nao katika kuandaa."
"Sawa mama!"

"Nakuona unameremeta tu, sitaki utoke na wala sichelewi narudi mchana huuhuu nikukute!"
"Sawa mama!"
Aliitikia Juliana huku akiwa ameshapendeza bila mama yake kujua kuwa wapo safari moja huko aendapo.


Kitendo cha mama Juliana kutoka kuelekea kupanda bodaboda hadi kituo cha Mwenge ndipo akapande daladala za kwenda Bagamoyo, huku nyuma Juliana alizuga kwa dakika chache na kuufunga mlango kisha akampigia simu Bitungu.
"Haloo"
"Ndiyo sweet!"

"Mbona hukunipigia tena ulipomaliza kuongea na bosi wako!"
Juliana alimtega Bitungu makusudi.
"Ohh! Sorry Sweet, nilijisahau hata hivyo simu yangu inaelekea kuisha chaji muda si mrefu itakatika na huku nilipo hakuna umeme!"
"Jamani! Hata Jenereta hamna baby!
"Ndiyo..."

Kabla Bitungu hajamalizia kuongea akaikata simu na kuizima kwa makusudi, alijua ameshamdanganya Juliana na wala hawezi kujua lolote. Alijiweka sawa akimsubiri mama Juliana. Aliamini baada ya muda ataiwasha simu na kumuelekeza alipo.

Kwa upande wa mama Juliana presha ilikuwa juu, alionyesha kuchanganyikiwa. Alishafika kituoni Mwenge na kumpigia simu Bitungu ikawa haipatikani, akashindwa afanye nini.
"Ndiyo nini ananifanyia! Kama alikuwa hataki kuonana na mimi leo si angeniambia?"
Alijisemea mama Juliana huku hasira zikimzidi, hakuonyesha kukata tamaa kwa sababu maji alishaamua kuyavulia nguo, alichokifanya aliendelea kupiga simu ya Bitungu mara mbilimbili huku ikiwa haipatikani, mara ikaita.

"Haloo!"
"Tushaonana watoto sasa!" Aliuliza mama Juliana kwa jazba.
"Hapana chaji mpenzi, vipi umefika wapi?"
"Nipo kituoni Mwenge, tena una bahati nilikuwa nataka kurudi nyumbani nikalale!"
"Ahhaa!! Usinifanyie hivyo mpenzi utaniua panda daladala uje!"
"Nishuke wapi!"

"Shuka Bagamoyo mwisho, nitakuja kukuchukua stendi, halafu tuelekee hadi eneo ilipo gesti."
Maneno yale yalimpa faraja moyoni mama Juliana, aliona anapendwa kuliko hata mume wake anavyompenda, mwili wake ulikuwa umepatwa na mshtuko kama wa radi na Bitungu tu ndiyo alikuwa fundi wa kurekebisha mshtuko huo. Haikuchukua muda mama Juliana akawa ameshaingia kwenye daladala ya kuelekea Bagamoyo.

Wakati mama Juliana akiwa ndani ya daladala, Juliana naye alikuwa tayari ameshauona mchezo mzima pale kituoni, alikodi bodaboda ya kumpeleka hadi Bagamoyo.
"Hakikisha daladala ile pale mbele yetu haituachi hata chembe!"
Juliana alimwamuru dereva bodaboda.

Kila kituo daladala ilipokuwa ikisimama, dereva bodaboda alikuwa akisimama kwa nyuma yao kidogo. Baada ya mwendo wa zaidi ya nusu saa hatimaye wakaingia Bagamoyo.
"Tusimame hapahapa!" Juliana alimuamuru dereva.

Mahesabu ya Juliana yalikuwa sahihi, alishuhudia mama yake akishuka kwenye daladala moja kwa moja na kufuatwa na Bitungu ambapo walikumbatiana kisha wakaingia kwenye bajaji na kuchomoka.
"Tuwafuate, mpaka nitajua mwisho wake, haiwezekani nifanyiwe mchezo mchafu huku nashuhudia!"
Aliongea Juliana huku dereva bodaboda akiendelea kuwafuatilia bila kujua kama anayemfuatilia Juliana ni mama yake mzazi.

Baada ya mwendo mfupi, ile bajaji ikawa imeshasimama, mama Juliana alitoka sambamba na Bitungu na kuelekea katika gesti ya Tupendane.
"Nimerudi tena!!"

Aliongea Bitungu, akimwambia mhudumu wa mapokezi katika ile gesti huku akielekea kwenye chumba alichopangiwa na kufikia moja kwa moja kwenye kitanda.
"Mpenzi nilikwambia huku kumetulia!"
"Kweli, lakiniii..."

"Lakini nini tena!! Umeshaanza kulalamika!"
"Hapana Bitungu, itabidi tufanye haraka nirudi si unajua huku ni mbali!"
"Najua!"

Mama Juliana alivua nguo zake na kufungua kimkoba alichokuwa nacho na kutoa khanga na kuivaa, kisha akatingisha mwili wake kwa makusudi mbele ya Bitungu aliyekuwa akimtolea macho.
"Twende basi tukaoge mpenzi!"
"Mhh, unajua wewe ni mzuri asikwambie mtu! Utamu ulionao ni zaidi ya kitu chochote!"
Aliongea Bitungu huku akivua suruali yake na kuchukua taulo la gesti na kumshika Mama Juliana hadi bafuni kwenda kuogeshana.

Muda wote Juliana alikuwa yupo nje ya gesti ya Tupendane, presha kwake ilikuwa kubwa, hakujielewa ni njia gani atatumia kujua chumba walichokuwa Bitungu na mama yake mule ndani.
"Kuna vyumba!"

Aliongea Juliana akimwambia mhudumu yule wa mapokezi.
"Ndiyo, unataka single au double?"

"Kwanza shilingi ngapi? Na ingekuwa vizuri kwanza niweze kuviona na ukubwa wake!"
Aliongea Juliana huku akijijua kabisa hakuwa na uwezo wa kulipia chumba kutokana na pesa kidogo aliyokuwa amebeba. Yule mhudumu wa mapokezi alimwelekeza chumba kimoja baada ya kingine huku akikiruka kile chumba ambacho yupo Bitungu na mama yake.
"Mbona vingine hunionyeshi?"

"Ukiona hivyo ujue vina watu ndani yake."
"Kwani?? Yule mama aliyeingia humu ndani na kijana mmoja hivi kama dakika kumi zilizopita kaingia chumba gani?"

Juliana alimuuliza yule mhudumu kimitego.
"Chumba hiki hapa tulichokiacha!"

Alijibiwa Juliana huku akili yote ikimuhama, akaachana na yule mhudumu na kuelekea chumba alichokuwa ameelekezwa, moja kwa moja akaufungua mlango wa kile chumba, haukuwa umefungwa hivyo akaingia moja kwa moja na kuzama ndani.
"Lakini huko si nimekwambia kuna watu!"
"Hata kama!! Nawafahamu ngoja niwasalimie kwanza!"

INAENDELEA.
Powered by Blogger.