KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Ni Shiida! Sehemu Ya Kumi naSita (16)

 LOVE STORY: ni shiidaI - 4
"Hata mimi Sweet wangu, siwezi kuisahau mechi ya leo. Si unakumbuka hata uwanja tuliochezea, yaani hapa nimejilaza hoi sijiwezi natamani ungekuwepo ungenikandakanda kwa maji ya vuguvugu."
Mama Juliana aliisoma meseji hiyo na kuiangalia mara mbilimbili kwa hasira za juu. Akajiongeza kuwa huenda Bitungu amechoka zaidi kwa kukutana na Juliana japokuwa hakuwa na hakika zaidi ya kuifananisha harufu ya pafyumu. Akamwandikia tena Bitungu meseji.

"Baby wangu hivi ile pafyumu yako inaitwaje tena? Maana nimeipenda harufu yake nataka kesho nikainunue ili nikiwa naitumia niwe nakukumbuka."
Mama Juliana alikuwa mjanja wa maneno, aliweza kuyaungaunga na kumdanganya Bitungu. Akaingia kwenye mstari na kumjibu.

"Waaaaooh! Sweet wangu, ina maana leo hii umeisahau? ile inaitwa UDV."
Meseji ikamfikia mama Juliana. Ikamuuma sana baada ya kujua ni UDV ambayo harufu yake ni ile aliyoisikia kwa Juliana. Alichotaka kujua ni kupata uhakika wa jina la pafyumu. Aliondoka pale sebuleni na kuongoza moja kwa moja hadi chumbani kwa Juliana. Akamkuta amejitupa kitandani huku akiendelea kulia kwa uchungu.

"Wee Juliana? Embu acha uchuro wako hapa!"
Aliongea mama Juliana huku akifuata mkoba ule wa Juliana na kuanza kupekua ndani yake. Jicho lake likagongana na kichupa cha pafyumu. Pafyumu iliyokuwa ikimuumiza kichwa. Pafyumu ya UDV.
"Wee Juliana! Juliana?"


Aliita mama Juliana kwa ukali.
Ndiyo kwanza Juliana aligeukia upande wa pili huku akiendelea kulia kwa maumivu, maumivu yale ya kipigo kutoka kwa baba yake. Ilibidi Mama Juliana atumie nguvu za mikono na kumvuta kwa nguvu.
?Mama niacheee!!?

?Si nakuita we mwanaizaya! Kumbe ulikuwa ukinisikia hutaki kuitikia, si ndiyo??
?Hapana mama, sijiskii vizuri mwili wote unaniuma!?
?Hata kama unakuuma, ujue Juliana!?

Mama Juliana akapunguza sauti na kuifanya isikike kwa chini ili mumewe asije akasikia kinachoendelea. Lengo lake ni kumuweka Juliana kwenye kumi na nane ajibu kila kitu kuhusiana na ile pafyumu aliyoitoa kwenye mkoba wake. Pafyumu ya UDV.
?Nakusikia mama!?

Juliana alijiweka vizuri. Hakuwa amebadili nguo tangu ametoka Bagamoyo alipokuwa na Bitungu. Alishusha miguu yake kwenye kitanda kisha akakaa.
?Nakusikia mama.?

?Mwanangu hivi kwa nini unapenda kufanya kitu kwa makusudi? Si nilikwambia usitoke??
?Ndiyo mama ila walikuja marafiki za...?
?Hivi mara ngapi haohao marafiki zako wanakupotosha we bado unafuatana nao. Kwa nini wewe usiwapotoshe mpaka wao ndiyo wakufanyie hivyo. Halafu mwanangu mpendwa unajua kabisa baba yako ana hasira.
?Najua mama.?

?Kama unajua kwa nini sasa mwanangu unakosea!?
?Nisamehe mama!?
?Mimi nilishakusamehe hata kabla baba yako hajakuchapa na mkanda. Ila mwanangu naomba uniambie mimi kama mama yako.?
?Nakusikia mama.?
?Una mpenzi??

Juliana alionyesha kushtuka. Alisogea kwenye kile kitanda. Woga ulimshika kwa muda huku macho akiyatoa.
?Hapana mama, bado najitunza!?
?Kweli unajitunza mwanangu Juliana??

?Ndiyo mama wala usiwe na wasiwasi na mimi!?
?Sasa mwanangu usiku wote huu tangu mchana ulikuwa wapi??
?Marafiki mama...?

?Haya hilo tuliache, mwanangu hii pafyumu nani aliyekununulia??
Juliana alishtuka kwa mara ya pili. Aliona sasa huenda mama yake alimuona kipindi kile Bagamoyo akiwa katika kupanda bajaji katika ile gesti alipokuwa na Bitungu. Mama Juliana alimuonyeshea Juliana ile pafyumu.

?Mama hiyo niliinunua mwenyewe!?
?Wapi? Na nani alikupa pesa??
?Nilijibanabana mama.?

?Hii ni pafyumu ya kiume mwanangu na wewe haikufai.?
?Nimekuelewa mama ila miye niliipenda harufu yake...?

Wakiwa katika majibizano, bila hata ya hodi mara baba Juliana akawavamia. Baba Juliana aliyekuwa ameshikilia simu mbili, moja yake moja ya mke wake. Kitendo cha kuingia akamkuta mama Juliana akiwa bado ameishikilia ile pafyumu huku akiwa amemnyooshea Juliana.

?Ina maana huyo mpuuzi bado hajalala siyo??
?Jamani! Nina maongezi naye kidogo ila atalala tu.?
?Na hiyo pafyumu uliyoshika ndiyo maongezi yanaingia vizuri siyo??
?Hapana mume wangu.?

?Embu leta, leta!?
Baba Juliana akaiwahi ile pafyumu na kumpokonya mkewe. Akawa ameshagundua kuwa ni ya kiume.
?Haya mnaweza kunieleza hii ya nani??
Wote kimya...
?Si naongea na wewe mama Juliana??
?Mume wangu embu basi punguza hizo hasira.?

?Msinichanganye? Ni nani anayetumia pafyumu ya kiume kati yako na Juliana??
Juliana aliendelea kutetemeka. Alijihisi kojo kumtoka kwani tayari kitumbua kilikuwa kimedondoka katikati ya mchanga, aliona ni bora alivyogundua mama yake kuwa ni ya kiume kuliko alivyogundua baba yake.

Alikuwa katika kusitasita huku akitaka kusema ukweli wote kuhusu uhusiano wake na mama yake pamoja na Bitungu ili litakalotokea litokee.
?Hiyo pafyumu alin...?

Kwa haraka mama Juliana alichezwa na machale. Akamuwahi Juliana kabla hajamalizia kuongea.
?Mume wangu hii hapa nimeipata huko kwenye vikoba nasikia ni nzuri kwa mabinti hasa mtoto wetu huyu, ndiyo nikawa nimemletea kama atapendezwa na harufu yake nimuachie.

INAENDELEA
Powered by Blogger.