KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Ni Shiida! Sehemu Ya Kumi na Kumi na saba (17)

 LOVE STORY: ni shiidaI - 4
Unasemaje mama Juliana? Ina maana ushaniona mtoto siyo? Haya sawa umemletea mwanetu safi! Embu nielekeze ni wapi wanapouza pafyumu ikiwa robo??

Kabla mama Juliana hajajibu, simu ikaita. Baba Juliana akaangalia mkononi na kugundua ni simu ya mama Juliana ndiyo ilikuwa ikiita huku jina likiandikwa Bitu. Akaichukua na kuipokea kisha akakaa kimya bila kuongea.
***
Muda wote Bitungu alikuwa hana raha. Aliwaza sana maneno aliyoambiwa mara ya mwisho na mama Juliana. Maneno juu ya pafyumu. Akili zote zilimuhama na kuona huenda anajuana na Juliana.
?Haiwezekani? Lakini kwa nini aniulize habari za pafyumu??

Alijiuliza Bitungu na kujijibu mwenyewe kisha akainuka pale kitandani na kuelekea kwenye meza ambapo aliiweka ile pafyumu yake ya UDV. Alipofika hakuona chochote.
?Ina maana kuna mchezo nafanyiwa au? Sasa itakuwa wapi??

Bitungu aliendelea kujiuliza mwenyewe. Alichokifanya aliichukua simu yake na kuanza kupiga namba ya mama Juliana. Iliita bila kupokelewa hadi ikakata, akajaribu kupiga kwa mara nyingine tena ikapokelewa.
?Mpenzi wangu mbona hupokei simu yangu? Embu niambie pafyumu yangu ya UDV uliichukua?



Bitungu aliendelea kufloo lakini bado upande wa pili hakujibiwa kitu chochote zaidi ya kimya kutanda. Alichokifanya aliikata simu na kuipiga kwa mara ya pili. Napo ikapokelewa tena na kumfanya atabasamu.


"Sweet wangu nitakuchukia? Embu niambie kama nimekuudhi nisamehe jamani bado nakupenda na sitaki kukupoteza hata kidogo!"

Bitungu aliendelea kuchanika maneno ya kimahaba bila hata kujua kinachoendelea upande wa pili. Safari hii aliipoza zaidi sauti yake huku akiwa amejilaza juu ya kitanda cha gesti na kuendelea kutoa sauti ya kubembeleza.


Akiwa katika kubembeleza bila kujibiwa mara akasikia makelele ya majibizano kati ya mume na mke yakiendelea. Akainuka harakaharaka pale kitandani akiwa hajiamini kwa kinachoendelea. Akaisogeza tena simu yake sikioni na kuendelea kusikia majibizano yale.


***Ugomvi uliendelea kuwa mkali kati ya baba Juliana na mkewe. Simu iliyopigwa na maneno yaliyokuwa yakiongelewa yalizidisha hasira za baba Juliana. Alijiangalia mara mbilimbili mwili wake ulivyotota kwa jasho na meno yakiumana kisha akamgeukia mkewe huku akimkazia macho na vidole akimnyooshea.


"Nikisema nianze kukutandika kama mtoto wako huyo nitakuwa nimekosea?"
"Kwani nimekosa nini mume wangu?""Si simu! Unajifanya hujui kinachoendelea?"
"Imefanyaje? Kwani we huwa hupigiwi simu na watu waliokosea namba?"


"Mama Juliana? Hivi ni mtoto gani utamdanganya kwa hiki kinachoendelea kwenye simu?"
"Mume wangu, leo unaonekana kuwa na hasira sana. Hiyo namba kubaliana na mimi kuwa imekosewa na imekuja kwa bahati mbaya.""Nakujisevu imejisevu kwa bahati mbaya siyo!"


"Kwani imejisevuje mume wangu si namba tu imetokea!"
"Batu sijui Bitu! Si umeandika wewe hapa unajifanya hujui siyo?"
Baba Juliana alimsogezea kwa ukaribu mama Juliana na kuanza kumwonyesha jina la Bitu kwenye ile simu yake. Simu haikuwa imekatwa hali iliyomfanya mama Juliana ashtuke na kutaka kuikata lakini baba Juliana akamuwahi na kuusogeza mkono wake pembeni.


"Unataka kufanyaje? Si umesema amekosea! Sasa kuanzia sasa hii namba nakula nayo sahani moja ama zangu ama zake pumbavu!""Msimamo wangu uko palepale mume wangu, siwezi kukusaliti hata siku moja na hiyo namba imekosewa.


Kama ukichukua maamuzi mabaya shauri yako wala usinishirikishe!"
"Nitaelewa tu msaliti ama siyo msaliti ngoja nilifanyie kazi. Kukuachia uhuru na mtoto wako mnautumia vibaya!""Amua utakavyofanya na ukweli utaujua maana nakwambia sijui lolote unaendelea kukazania, amua tu!"


Iliimbidi mama Juliana azuge kuwa amekasirika ili baba Juliana aamini lakini wapi! Ndiyo kwanza baba Juliana aliondoka chumbani mule na kumuacha Juliana na mama yake wakiwa kwenye butwaa. Vita ikaanza upya kwa Juliana na mama yake.

INAENDELEA
Powered by Blogger.