KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mwajuma Mtamu Sehemu Ya Kumi Na Moja (11)

Kipindi hicho bado nilikuwa nikiishi nyumba moja na Savela, tangu alipoweza kunisaidia na kunishawishi mpaka nikajiingiza katika biashara ya uchangudoa.
Jambo ambalo wengi wenu hamlifahamu kuhusu hii biashara ya uchangudoa ni biashara kama zilivyobiashara nyingine. Kuna wakati unaweza ukapata hasara au faida.

Hakuna kipindi kigumu ambacho biashara inakuwa ngumu kufanyika kama kipindi cha hedhi, pale tunapokuwa katika siku zetu. Tunapata maumivu makali sana.

Kila msichana anayejihusisha na biashara hii ya uchangudoa sikufichi kitu ambacho tunakichukia ni kwenda hedhi kila mwezi.
Kipindi hicho biashara inakuwa ngumu kufanyika, maisha yanabadilika na ndiyo kipindi ambacho huwa tunasaidiana mpaka pale tunapokuwa sawa na biashara kuendelea kama kawaida.


Nilikuwa nikifanya mapenzi na wanaume wanne na wakati mwingine nilikuwa nikifanya na wanaume sita kwa siku. Walikuwa wakinilipa vizuri.
Kwa siku nilikuwa sikosi si chini ya laki moja na nusu, biashara ya siku hiyo ikiwa nzuri zaidi nilikuwa naingiza laki mbili.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu kwa wakati huo, sikujali nililala na mwanaume wa aina gani, mwenye umri upi, mwembamba, mnene, mfupi au mrefu.

Yoyote aliyejitokeza mwenye pesa nilienda kulala naye bila kujali lolote, nilihakikisha nafanya naye mapenzi kama sikutakiwa kufanya tena katika maisha yangu.
Nilitengeneza kiasi kikubwa cha pesa tena ndani ya muda mfupi.Savela alionekana kukubuhu katika biashara ya uchangudoa, kipindi ambacho nilikuwa nikienda Sinza kujiuza yeye alibaki nyumbani, wanaume walikuwa wakimfuata.
Sikutaka kuendelea kuishi nyumba moja na Savela, kwa kuwa nilifanikiwa kutengeneza kiasi kizuri cha pesa nilipanga kupanga nyumba yangu.
Nilipomwambia Savela kuhusu mipango hiyo alionekana kufurahi, alinipongeza kwa hatua nzuri ambayo nilikuwa nimefikia.
"Kwahiyo umepanga kuishi wapi?" aliniuliza.
"Sinza," nilimjibu.
"Sawa," aliniambia.
Baada ya siku kadhaa kupita, nilitafuta dalali ya nyumba ambaye nilimuelezea nyumba niliyokuwa nikiihitaji.
Dalali alionekana kuifahamu Sinza kiundani, baada ya kunisikiliza kwa muda mfupi akaniambia nyumba ilikuwepo tena kama ningezembea kuna mtu mwingine alikuwa akiihiitaji.

"Iko wapi?" nilimuuliza.
"Sinza kwa Remi," alinijibu.
"Ni nzuri na itaendana na mimi?" nilimuuliza.
"Ndiyo tena itaendana na hadhi yako," alinijibu.
Sikutaka kupoteza muda, nilienda naye mpaka kwenye nyumba hiyo ili nione kama kweli yale aliyokuwa akinieleza kuhusu nyumba hiyo yalifanana.
Kweli bana nilipofika nilikuta kila kitu nilichokuwa nikikihitaji katika nyumba, ilikuwa ni nyumba ya vyumba vitatu, sebule, chumba, jiko pamoja na choo.

"Umeipenda?”
"Ndiyo nimeipenda, ni nyumba nzuri."
Baada ya makubaliano na dalali alinikutanisha na Mama mwenye nyumba hiyo, aliyejulikana kwa jina la Bi Latifa. Nilipokutana naye alinieleza kila kitu kuhusu nyumba yake, haikuwa na tatizo lolote na aliniambia angenipangishia kwa shilingi laki mbili na nusu kila mwezi.

"Laki mbili na nusu?" nilimuuliza.
"Ndiyo tena nimekupunguzia baada ya kukuona, nilikuwa naipangisha kwa laki tatu au Jafari hujamwambia?" aliniambia huku akimuuliza yule dalali.
Kwa kuwa nilikuwa nina shida na uhitaji mkubwa wa nyumba kwa wakati huo sikutaka kuweka longolongo nyingi, nilichoamua kukifanya ni kuingia mkataba na Bi Latifa.
Nilimlipa kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano, kodi ya miezi sita kama mkataba alivyokuwa ukisema. Bi Latifa alifurahi sana baada ya kumpatia kiasi hicho cha pesa.

Hatimaye niliyaanza maisha mpya katika nyumba hiyo, nilinunua kila kitu kilichokuwa kikihitajika ndani ya nyumba.

Kwa maisha niliyokuwa nikiishi ilikuwa ni vigumu mtu kuamini kama nilikuwa ni changudoa ambaye nilivizia usiku ndipo niende kufanya biashara hiyo.

Inaendeleeaaa
****

Powered by Blogger.