KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mwajuma Utamu Sehemu Ya Kumi (10)

Mazungumzo yaliyokuwa yakizungumzwa mahali hapo yalikuwa ni ya kibiashara, Ibra muda wote alikuwa akanitazama.

Nilitakiwa kufanya biashara ya uchangudoa na nilikubali kuifanya hivyo kila kitu kilichokuwa kikiendelea nilikubaliana nacho bila wasiwasi wowote, niliamini ilikuwa ni biashara ambayo ingeweza kunipa utajiri wa haraka.

"Kwahiyo mnakula nini?" aliuliza Ibra wakati huo alimuita muhudumu akawa anasubiria oda yetu.
"Mimi niletee mchemsho wa ndizi nyama," alisema Savela.
"Mimi niletee chochote tu," nilijibu jibu lililowafanya wote wakacheka.
"Hakuna chakula hicho, wewe sema unataka chakula gani?" aliniuliza Ibra.
"Basi niletee Chips," nilisema.

"Chips nini, kuna mayai, kuku, mishikaki au kavu unataka?" aliniuliza yule muhudumu, alikuwa ni wa kiume.
"Chips mayai," nilimjibu kisha akamgeukia Ibra na kumuuliza huduma ya chakula ambacho alihitaji.

"Hapana nipo sawa aisee, wewe wahudumie hawa warembo tu usijali," alijibu kisha yule muhudumu akaondoka, baada ya dakika kadhaa alirudi na vyakula tulivyomuagiza.
Tulianza kula huku stori za hapa na pale zikiendelea, Savela aliniambia siku hiyo nilitakiwa kwenda kulala na Ibra.
Kiukweli kila nilipokuwa nikimuangalia Ibra jinsi alivyokuwa akionekana halafu nilipokumbuka kuwa usiku huo nilitakiwa kwenda kulala naye nilihisi kuingiwa na uwoga.

"Hutakiwi kuogopa kitu Mwajuma halafu tafadhali naomba usiniangushe," aliniambia Savela.
"Sawa dada siwezi kukuangusha," nilimwambia kisha tukaendelea kula mpaka pale ambapo tulimaliza, Ibra akalipa bili ya chakula.
"Kwahiyo nini kinachofuata?" aliuliza Ibra huku akimtazama Savela, hapohapo nikamuona Savela akinipa ishara ya kuniambia niondoke na Ibra.
"Nitamrudisha asubuhi," alisema Ibra kisha akanishika mkono tukaanza kuondoka.

"Sawa hakuna shida," alisema Savela.
Tulifika mpaka alipokuwa amelipaki gari lake, tukapanda kisha tukaondoka.
****
Safari yetu iliishia nje ya hoteli moja ya kifahari iliyokuwepo maeneo ya Sinza Makaburini. Hatukutembea umbali mrefu sana kutokea Sinza Afrika sana, ulikuwa ni mwendo kama wa dakika kumi na tano hivi tukawa tayari tumeshafika katika hoteli hiyo.
Ibra hakutaka kupoteza muda, alichukua chumba na baada ya muda mfupi tukaingia ndani ya chumba hicho. Kila nilipokuwa nikimtazama Ibra nilikuwa nikiogopa, niliingiwa na wasiwasi, nilitamani masaa yakimbie ili niondoke mahali hapo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulipokuwa ndani ya chumba cha hoteli hiyo hakukuwa na stori nyingine alizoziongea Ibra zaidi ya mapenzi, umbo langu lilionekana kumchanganya kupita kawaida, muda wote alikuwa akinisifia.
"Umewahi kulala na wanaume wangapi katika maisha yako?" aliniuliza.
"Watatu tu," nilimjibu.
"Kumbe mtoto bado mbichi kabisa?" aliniuliza.
"Ndiyo," nilimjibu.
"Leo nataka uniliwaze, nataka unipe mapenzi mpaka nimsahau mke wangu huko alipo," aliniambia huku akitabasamu.
"Kumbe una mke?" nilimuuliza kwa mshangao.
"Ndiyo nina mke lakini naishi kama sina mke."
"Kivipi?"
"Amepooza hivyo naishi naye kama sanamu tu, siwezi kufanya lolote lile," aliniambia huku akiniomba tusiyazungumzie hayo.
Ibra hakutaka kupoteza muda, alianza kunipapasa huku akijaribu kunionyesha utundu aliyokuwa nao wa kunifundisha hesabu za 2x+3y.
Nilisisimka mwili, hata hivyo sikutaka kubaki kuwa kama mwanafunzi wakati somo lenyewe nilikuwa nalifahamu tena zaidi yake.
Nilikuwa nikifahamu mbinu na mahesabu yote ya kitandani. Hakukuwa na kitu kigeni kwangu, siku hiyo haikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kufanya mapenzi.
Kila kitu nilichokuwa nikikifanya kilimshangaza sana Ibra, hakutaka kuamini kama nilifahamu mambo yote yale.

Nisingependa kusimulia kila kitu nilichokifanya usiku huo kwasababu ya kuheshimu sheria za kimitandao ila nataka mfahamu kuwa siku hiyo nilifanikiwa kufanya mapenzi na Ibra tena kwa asilimia mia moja.
Asubuhi ya siku iliyofuata tuliamka kisha tukaenda kuoga kwa pamoja, tulipomaliza tulijiandaa tayari kwa kuondoka.

"Umenifurahisha sana mrembo, umenipa mapenzi ambayo sijawahi kupewa hapo kabla, hivi nani aliyekufundisha?" aliniuliza.
"Hakuna mtu aliyenifundisha kufanya mapenzi," nilimjibu kwa kujiamini.
Nilishangaa akitoa kiasi cha pesa kama laki mbili na nusu hivi kisha akanipa, nilipokea na kumshukuru.

"Hutakiwi kusema asante, hiyo ni haki yako," aliniambia huku akikenua.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kulala na wanaume tofauti tofauti, kila siku nilikuwa nikifanya nao mapenzi na walikuwa wakinilipa vizuri.

Katika kipindi hicho biashara ya uchangudoa ilionekana kuwa nzuri kwa kiasi fulani, ilikuwa ikinipa faida kubwa na lilikuwa ni jambo gumu kuiacha biashara hiyo kwani tayari ilikuwa ni sehemu moja ya maisha yangu. Kila kitu nilichokuwa nikikifanya, kuanzia kula yangu, kuvaa kwangu ilitokana na biashara hiyo.

Inaendeleaaaaa.....
Powered by Blogger.