KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mwajuma Utamu Sehemu Ya Nane (8)

Kwa muda ambao Savela aliutumia kuzungumza na mimi tayari alikuwa ameipandikiza mbegu ya tamaa ya mafanikio ndani yangu, alijua kunishawishi, alijua kuzungumza yaani maneno yake yalitosha kunifanya nitamani kujua ni biashara gani hiyo ambayo alikuwa akiifanya.

Siku ziliendelea kukatika huku ujauzito nao ukiendelea kukua, mwanzoni nilimficha Savela hali niliyokuwa nayo lakini kama unavyojua mimba haiwezi kufichika mwisho wa siku alifahamu kila kitu.

Hakuonekana kuchukia baada ya kufahamu ukweli ambao nilimficha hapo awali, alinikumbusha kuhusu msaada ambao aliamua kunipa ulikuwa ni wa lengo la kufanya biashara. Ilibidi nimuulize ni biashara gani hiyo ambayo kila siku alikuwa akinidokeza na ndipo hapo ambapo aliniambia ukweli, aliniambia biashara hiyo ilikuwa ni ya uchangudoa yaani ilitakiwa nijiuze ili niweze kupata pesa, alienda mbali zaidi na kuniambia kuwa mafanikio yake yote yalisababishwa na biashara hiyo uchangudoa.

Nilihisi mwili wote ukipigwa na ganzi baada ya kuyasikia hayo, sikutaka kuamini hata kidogo, kuna muda nilidhani labda alinitania lakini hakukuwa na utani kati yangu na yake.
“Baba wa huo ujauzito ni nani?”
“Ni Oscar.”
“Anajua?”
“Ndiyo ila anifukuza, aliukataa.”
“Sawa, sasa kwenye kazi hii ya uchangudoa ujauzito hautakiwi, utakupotezea wateja," aliniambia Savela.
Licha ya kuwa nilitokea katika maisha ya kimasikini pamoja na kukutana na changamoto zote mpaka kufikia hatua ya kukutana na Savela bado nilikuwa mwenye tamaa.
Tamaa ya utajiri ilishakwishaniingia, kila nilipokuwa nikimuangalia Savela pamoja na mafanikio aliyokuwa nao katika maisha yake sikutaka kuamini kama biashara hiyo ya uchangudoa ndiyo iliyomletea mafanikio yote hayo, kuna muda nilikataa lakini mwisho wa siku nilijikuta nikiamini.
Kwa kuwa nilikuwa tayari kufanya lolote Savela alinishauri niende hospitali nikautoe ujauzito niliyokuwa nao kwa madai kuwa ingeniharibia soko la biashara yangu ya uchangudoa.

Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, mipango ikaandaliwa kisha nikaenda kwenye hospitali moja ya kibinafsi maarufu sana hapa mjini, sitaweza kuitaja kwasababu za kibiashara.

Nilifanikiwa kuutoa ujauzito wa miezi mitatu, hilo lilimfurahisha Savela mno, aliniambia huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kutengeneza pesa na kuwa mwenye mafanikio kama aliyokuwa nayo yeye.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kichwa changu kilikuwa kikifikiria utajiri ambao ningeweza kuupata kutokana na biashara hiyo ya uchangudoa.
Hakukuwa kuna kitu nilichokuwa nikikitamani kama kuwa na maisha mazuri. Niliutamani sana utajiri, nilipokuwa nikimsikia mtu akipiga stori za pesa nilihisi kusisimka mwili.

Kipindi hicho biashara niliyoambiwa kuwa ingeweza kunipa utajiri wa haraka ilikuwa ni ya uchangudoa, nilitakiwa kujiuza kwa wanaume ambao wangenilipa na mwisho wa siku maisha yangu yangeweza kubadilika.
Mwanzoni biashara hiyo ya uchangudoa haikuniingia akilini, niliogopa kuifanya lakini Savela aliendelea kunishawishi.
Siku moja majira ya usiku alinipeleka Sinza kwenye klabu moja maarufu sana, Ambiance. Ilikuwa ni sehemu maarufu kwa wasichana kufanya biashara hiyo ya uchangudoa.

Macho yangu hayakutulia sehemu moja, nilikuwa nikiyashangaa mazingira niliyokutana nayo mahali hapo, wakati huo tulikuwa tumekaa nje ya baa hiyo upande ambao niliweza kuiona barabara ya Shekilango.
"Unashangaa nini?" aliniuliza Savela, wakati huo alikuwa ameagiza pombe kwa muhudumu aliyekuja kutusikiliza.

"Hakuna kitu," nilimjibu huku nikijiweka sawa.
Muhudumu huyo akanigeukia na kuniuliza kuwa nilihitaji nini kwa muda huo, sikuwa ni mtumiaji wa kilevi chochote, nilimuagiza soda.
Jibu hilo likamshangaza sana Savela, akazidi kuniona nilikuwa mshamba sana.
"Hutumii pombe?" aliniuliza, muda huo yule muhudumu alikuwa tayari ameenda kuleta vinywaji.
"Ndiyo situmii," nilimjibu.
"Kwanini?"
"Sijazoea."
"Mmh!"
Baada ya dakika kama tatu hivi yule muhudumu aliweza kurudi na vinywaji, alipomaliza kutuhudumia nikashangaa akimsogelea Savela, akamnong'oneza kitu, nikamuona Savela akitabasamu. Sikufahamu kwa muda huo ni nini kilichokuwa kikiendelea.

Nilianza kuinywa soda yangu taratibu huku nikiendelea kuyashangaa mazingira ya sehemu hiyo. Kwa mbali niliwaona wasichana watatu waliyokuwa wamevalia mavazi yaliyowaacha sehemu kubwa za mwili wao kuwa wazi, walikuwa wakiikimbilia gari iliyokuja na kupaki eneo hilo la baa, walikuwa wakigombaniana, kila mmoja alihitaji kuwa karibu na kioo ambacho kilifungiliwa na dereva wa gari hilo.

Inaendeela...
Powered by Blogger.