KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Ni Shiida! Sehemu Ya Nane (8)

 LOVE STORY: ni shiidaI - 4
Ilikuwa katika hali ambayo hakuitarajia kabisa, Juliana aliona hereni chini kando ya kitanda. Hereni hiyo alivyokumbuka ni moja ya hereni alizomnunulia mama yake miezi miwili nyuma.
"Mh!" aliguna Juliana huku akiiokota. Akajiuliza…"Au mama alipokuwa huku Sinza aliingia hapa nini?"
Lakini alipata wazo kwamba asiichukue, aiache palepale chini ili aone kitakachotokea kama Bitungu ataiona.

Bitungu alitoka chooni kwa kujiamini sana, akakaa kitandani. Lakini na yeye jicho lake likatua moja kwa moja kwenye ile hereni ambapo alionekana kushtuka sana.Kama vile haitoshi, kwa sababu Juliana alilala, yeye alikaa, aliinuka na kuifuata kiaina huku akikumbuka…

"Hii hereni si ndiyo alisema yule mama kwamba ameipoteza, kumbe iliangukia hapa?"
Wakati anaifuata hereni hiyo, Juliana alimwona, akashtuka zaidi kwani sasa alijiridhisha kwamba alichokifikiria ndicho."Lakini huyu si alikuja kuchukua chumba sasa hivi, sasa hereni inamhusu nini? Au na yeye anashangaa kuona hereni ndani ya chumba?" aliwaza Juliana akakaa mkao wa kusubiria atakachosema Bitungu lakini hakikuwepo.

Ghafla Juliana alikosa amani ndani ya moyo wake. Alianza kuingiwa na wasiwasi na hofu ya mambo mengi akivuta matukio kadhaa ya nyuma."Inawezekana mama anatembea na Bitungu? Hilo haliwezekani hata kidogo, yaani Bitungu alale na mimi na mama yangu?"

"Baby vipi?" Bitungu alimuuliza Juliana huku na yeye akipanda kitandani. Juliana alipoitika poa, aliinuka kitandani kiaina na kuangalia ile sehemu aliyoiona hereni, haikuwepo!"Mh!" aligunia moyoni Juliana, alikosa nguvu na raha.

"Baby, mbona kama umekosa raha ghafla?" aliuliza Bitungu akijipendekeza kwa kumshikashika Juliana sehemu mbalimbali za mwili wake."Usinishike bwana, nini?" alikuja juu Juliana. Ni kweli alikosa raha kwani asingeweza kusema maneno hayo kama angekuwa na amani…
"Ha! Ina maana yamekuwa hayo leo mpenzi wangu?" aliuliza Bitungu…
"Ndiyo ee..."

"Kosa langu ni nini..?"
"Unalijua mwenyewe."
Bitungu alijaribu kujiongeza akiamini anaweza kupata mwanga au jibu lakini wapi! Hakuona kosa lake.
Mara, mlango uligongwa na mhudumu, Bitungu akaenda kufungua…
"Samahani kaka, kumbe ni wewe, nilifikiri kaingia mtu mwingine."


"Ni mimi?"
"Lakini ulitoka umerudi tena?" aliuliza mhudumu swali ambalo lilimshtua Juliana pale kitandani.
"Mh! Ina maana kumbe Bitungu alikuwemo humu ndani? Mbona mimi aliniambia anakuja kutafuta chumba alipokipata ndiyo akaniita tuje?" alijiuliza Juliana.

Bitungu hakujibu swali la mhudumu huyo badala yake alifunga mlango tu na kurudi kitandani…
"Baby," aliita Juliana…
"Yes baby…"

"Kumbe ulikuwemo humu ndani?"
"Hapana, amejichanganya yule."
"Mm! atajichanganyaje bwana, we ulikuwemo humu na uniambie ukweli ulikuwa na nani?"
"Baby, mimi sikuwemo humu ndani ya chumba, yule amejichanganya tu, naomba unielewe."
"Hamna bwana, mimi tayari kuna mambo yameniambia ulikuwemo."

"Mambo kama yapi?"
"Wewe unajua mwenyewe."
"Khaa! Mimi sijui mbona."
"Basi yaishe," alisema Juliana na kumfanya Bitungu ajisikie vibaya zaidi kwani na yeye alianza kuhisi kwamba ile hereni aliyoiokota ya mama Juliana ilishaonwa na mrembo huyo ndiyo maana amepoteza furaha kwa ghafla kuliko alivyoingia…

"Yaishije baby wakati najua kwako bado?"
"Yaishe tu! Halafu leo mimi tumbo linaniuma kwelikweli, wala sijisikii kufanya kitu chochote kile," alisema Juliana kauli iliyompotezea dira Bitungu kwani alishajitiuni kwamba anakwenda kushinda mechi ya siku hiyo.

Bitungu ili ajue kama madai ya Juliana ni ya kweli au alitaka kutingisha kiberiti tu, alijifanya kuanza kumshikashika Juliana sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimchombezea kwa maneno matamu sana yenye kuchochea mahaba niue!

"Nimesema leo sijisikii kufanya chochote kile si nilishasema mapema lakini baby?"
"Aaa! Juliana, usinifanyie hivyo mimi."
"Mimi sijakufanyia baya lolote lile…"
"Ila..?"
"Basi tu."

"Sasa ikiwa ni hivyo tutafika mbali kweli baby wangu?"
"Hatuwezi," alisema Juliana kwa sauti iliyoendelea kuonesha kuwa, hakuwa sawa kichwani mwake.
Jitihada zote za kutaka kushinda mechi na Juliana ziligonga mwamba kwani mrembo huyo hakuwa tayari kwa njia yoyote ile."Bitungu," aliita Juliana kwa sauti iliyojaa utulivu wa hali ya juu…
"Yes."



ITAENDELEA
Powered by Blogger.