KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Ni Shiida! Sehemu Ya Tisa (9)

 LOVE STORY: ni shiidaI - 9
"Una uhusiano na nani?"
"Mimi?"

"Wewe ndiyo, mwingine nani?"
"Sina."
"Si kweli. Ile hereni ilikuwa pale iko wapi?"
"Hereni gani?"
"Pale chini palikuwa na hereni sasa hivi haipo, we umeiokota. Na ndiyo nathibitisha kwamba kweli wewe ulikuwemo ndani."

"Hapana, siijui mbona."
"Nikupapase?"Bitungu hakutaka kupapaswa kwani ni kweli aliiweka hereni hiyo kwenye mfuko wa bukta.
"Ina maana huniamini baby?"
"Ndiyo sikuamini. Tena kuna kitu nafuatilia kama ni kweli mimi na wewe basi."
"Kitu gani tena baby jamani?"
"Nakijua mwenyewe."
***
Mama Juliana alihisi dakika zinakatika binti yake hajarudi, akampigia simu.
Juliana alishtuka sana kuona simu ya mama yake ikiingia kwenye simu yake…
"Huyo ni mama, please naomba subiri kwanza kufanya lolote lile kwa sasa," alisema Juliana ili apokee simu hiyo…

"Mama…"
"Uko wapi wewe?"
Ili ajulikane yupo njiani anatembea, Juliana aliwahi kwenye dirisha na kuongelea hapo ili kelele za nje ya gesti hiyo ziingie kwenye simu na kumfikia mama yake…
"Mama natembea nakuja."
"Na huyo Bitte?"

"Hapana mama, nimemkuta ana kazi nyingi sana lakini atakuja kesho asubuhi sana."
Mama alikata simu, Juliana akamgeukia Bitungu…
"Naomba hiyo hereni Bitungu please."
"Yaani dear hayajaisha tu?"

"Hayawezi kwisha labda uamue kuwa wazi kwangu kuhusu mwanamke aliyekuwemo ndani na uhusiano wake na hiyo hereni uliyoiokota."
"Sikia nikwambie ukweli baby wangu…"
"Nakusikiliza."

"Ni kweli nilikuwa na mwanamke kabla yako. Lakini ni yule mke wa mtu niliyewahi kukwambia kwamba ananing'ang'ania mimi simtaki."
"Ulikuwa naye humu ndani ya chumba hiki?"
"Ndiyo."

"Mnafanya nini?"
"Yeye alichukua hiki chumba, akaniita akisema anataka kunipa kazi nimfanyie ili anipe pesa lakini si suala la mapenzi."

"Amekupa hiyo kazi?"
"Ndiyo.""Kwanza huyo mwanamke anaitwa nani?"



?Mh! Jina lake linanitokaga sana.?
?Kwa nini ushindwe kumjua mtu anayekufuatafuata kila wakati mpaka mnaitana gesti??
?Imetokea tu.?
?Anaishi wapi??

?Mwenyewe anasemaga Ilala.?
Moyo ulimlipuka Juliana, alianza kuuona ukaribu wa mama yake kutembea na Bitungu. Alitamani sana kumuuliza lakini alishindwa, akaendelea kutumia maswali ili kumchimba kwa undani.
?Umewahi kufika nyumbani kwake??
?Sijawahi.?
?Ni Ilala gani??
?Sijui Ilala gani!?
?Yukoje??

?Mwanamke f?lani hivi hajatulia ndiyo maana mimi namkataa maana najua nitaangukia pabaya.?
?Ameolewa??
?Hapana, shangingi tu,? alijibu Bitungu kwa kukwepesha ukweli kwani alijua akikubali kwamba ameolewa, ataonekana anacheza na hatari kwa wake za watu lakini hakujua kama jibu hilo lilipunguza kiwango cha mawazo cha Juliana kutaka kumhusisha mama yake.
?Kwa hiyo humu chumbani ulikuwa na huyo mwanamke wako??
?Ndiyo.?

?Umesema ndiye aliyekodi chumba??
?Yes baby.?
?Kwa hiyo mimi umeniingiza kwenye chumba alichochukua mwanamke mwenzangu siyo??
?Juliana, punguza hasira mama, punguza maswali pia, usimuwazie sana huyo malaya, wewe shughulika na mimi tu, mimi ni mumeo mtarajiwa Juliana, mtoto mzuri kama wewe unataka kujilinganisha na mwanamke mtu mzima, mzee yule.?

Maneno hayo yalimpa faraja kubwa Juliana, akajijua tena kwamba kumbe yeye ni mzuri sana na anapendwa pia kumbe anaweza kuwa mke wa mtu ndoto ambazo zimekuwa zikimkaa kichwani muda mrefu kwamba atafurahi sana siku moja atakapobahatika kuolewa na kuwa nyumbani kwake.
Kwa mbali, Juliana alianza kuchangamka huku akipeleka mkono wake kumshikashika mwilini kijana huyo na kuachia tabasamu, akasema?

?Lakini ujue baby mimi ni msichana mwenye wivu mkubwa. Kwa hiyo uwe unaangalia unapotaka kunitenda kwani utakuwa unaniumiza sana.?

?Miye wala sikutendi mpenzi wangu, unajua kama ningekuwa na nia mbaya nisingekuita uje hapa.?
Bitungu naye baada ya kumwona Juliana amelegeza uzi aliitumia nafasi hiyohiyo kuhakikisha wanaangukia kitandani na kuanza mechi ya haraka maana dakika zilikuwa zimekatika sana.
?Jamani, nitalala mwenyewe,? alisema Juliana wakati akipelekwa kitandani?
?Si nakusaidia tu baby wangu jamani na wewe!?

?Nitajisaidia mwenyewe jamani sweet,? alilalamika Juliana kwa sauti isiyokuwa na msisitizo, akaenda kitandani na kuangukia puu!

INAENDELEAH
Powered by Blogger.