KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Ni Shiida! Sehemu Ya Tatu (3)

LOVE STORY: NI SHUDA - 3
Kumbe kwa Juliana, dakika arobaini na tano nzima za mchezo bado anakuwa moto, kuanzia hapo ndipo anaweza kutangaza kufika kwenye kilele cha mlima wanaoupanda. Sasa Bitungu yeye alizoea dakika saba au kumi za mchezo awe kama amecheza kipindi cha kwanza.

Ilikuwa wakati Bitungu yu hoi kabisa akitamani Juliana augue ghafla ili waache, ndipo alipotangaziwa kuwa sasa wafike wote lakini wakati huo kijana huyo alikuwa amejizuia kiasi cha kuwaza mambo mengine tena yale ambayo ni kero ili amudu kwenda na biti za demu huyo.

"Haa! Haa! Daa!" alikuwa akihema Bitungu huku Juliana akiwa katika pozi la kawaida sana kama vile alitoka kubeba godoro tu kutoka sebuleni kupeleka chumbani.
"We Juliana," aliita Bitungu…
"Abee…"
"Abee nani?" Bitungu aliuliza akitaka kujua kama bado anakubalika kuitwa baby au lilikuwa jina la kitandani tu!
"Abee sweetheart."

Bitungu akafurahi sana kusikia kwamba hata nje ya kitanda ameitwa jina zuri zaidi kimahaba…
"Hivi nani amekufundisha?"
"Nini?"

"Kufanya haya uliyonifanyia kitandani leo?"
"Mimi mwenyewe utundu wangu."
"Mh! Usiniache baby?" alisema Bitungu.
"Siwezi kukuacha dear labda uniache wewe. Mimi nataka tufike mbali sana zaidi ya hapa."
"Hata mimi, natamani ikibidi tufunge ndoa."
"Kweli sweet?"
"Sana tu."

Simu ya Juliana iliita tena…
"Mungu wangu…yaani huyo ni mama bila ubishi wala kujiuliza," alisema Juliana akiifuata simu yake…
"Si nilisema…sasa ngoja niweke loud speaker usikie mitusi yake," alisema Juliana huku akiiseti simu hiyo.
"We nguchiro usiyefaa kufungwa na binadamu, mwana wa shetani mtesa wanadamu, kenge mwenye mabaka uko wapi?"



"Nipo njiani narudi mama…"
"Nipo njiani narudi mama," mama mtu aliirudia kauli ya bintiye huku akiwa ameziba pua…
"Unarudi na ndege au gari dogo, mbona sisikii kelele?"
"Natembea kwa miguu mama. Si nilikwambia nipo hapa jirani."
"Nakuuliza mbona sisikii kelele?"

"Mama, mtaa huu watu wametulia sana, si kama hapo kwetu, ndiyo maana."
"Kwa hiyo unataka kuniambia wewe ni mwenyeji sana na huo mtaa kuliko mimi mama yako siyo?"
"Hapana mama."

Wakati Juliana anazungumza na mama yake, Bitungu alimsogelea hadi jirani ili kuisikiliza sauti hiyo vyema kama anayeijua…"Mh," aliguna Bitungu.

Baada ya kukata simu, Juliana alimuuliza ni kwa nini alimsikilizia kwa karibu sana…
"Sauti kama naijua kwa mbali."
"Kama ya nani?"

"Mtu mmoja hivi lakini najua siye," alisema Bitungu. Waliachana na hayo, Juliana alijiandaa harakaharaka na kuondoka baada ya kumpiga busu zito kijana huyo…
"Nitakumisi sana baby," alisema Juliana.
"Hata mimi."
***

INAENDELEAA
Powered by Blogger.