KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Simulizi : Shida Sehemu Ya Kumi na Nane (18). MWISHOO

Hadithi nzuri ya kusisimua ya shida
" Itabidi tushukie hapa ili nimtafutie kwanza huyu sehemu ya kufikia" aliwaza Kolumba Pale pale alimshika mkono Shida na wakaomba kushushiwa pale. Baada ya kushuka walipanda daladala na kuelekea Kimara mwisho huko wakashuka na kuchukua bajaji iliyowapeleka eneo moja ndani ya Kimara Baada ya muda walifika eneo husika na Kolumba alishuka na kumlipa mwenye bajaji kisha wakaingia kwenye nyumba moja yenye geti kubwa jekundu.

" Kolumba umepotea sana wewe kijana,nini kimekuleta leo hii?" aliuliza mama mmoja mtu mzima

" Mihangaiko ya maisha mama,af nashida na wewe njoo tafadhali" akasema Yule mama alisogea pale kalibu ili amsikilize Kolmba

" Mama huyu ni mgeniu wangu,anaitwa Shida yeye ndo atakuwa anaishi kwenye hiki chumba changu kwa muda" akasema Kolumba

" Haina shida kalibu dada" akajibu yule mama " Ahsante mama" akajibu Shida Kolumba alitoa funguo na kufungua mlango wakaingia ndani. Kilikuwa chumba kizuri sana kikiwa na kitanda kizur,tv,friji,feni na sofa ya mtu mmoja!

" Shida mimi siishi hapa ila hiki chumba nilikipanga kw ajili ya wageni wangu,ninapoishi ninaishi na wazazi wangu hivyo nisingeweza kwenda na wewe pale,naomba ukae hapa kwa muda wakati naangalia namna ya kukusaidia" Kolumba alimwambia

" Nashukuru sana kakangu,una moyo wa huruma sana" akajibu Shida na kwenda kumkumbatia Kolumba Baada ya muda Kolumba aliaga na kuondoka akimwacha Shida akiwa haamin kama amekutana na mtu mwema hivyoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" huyu alivyo mzuri hivi na alivyo na moyo wa huruma hivi hata akitaka awe wangu niko tayari, na hata ikibidi nitamtega ili awe wangu nifaidi maisha ya hapa Dar"

aliwaza Siku hiyo aliangalia tv mpaka usingizi ulipomptia. Asubuh ya siku iliyofata Shida aliamka saa tano baada ya kugongewa mlango na Kolumba aliyekuwa ameshafika. Alimfungulia na kukaa kitandani

" Huu ni mswaki wako,na dawa ile pale, kama hutajli chukua ndoo hiyo hapo ukaoge ili tutoke kidogo" akasema Kolumba Upande wa pili wa maisha halisi ya Kolumba alikuwa na mke na watoto wawili Hakuoa kwa kupenda bali alimpa mimba mtoto wa kigogo na kujikuta akilazimishwa kumuoa. Kolumba hakuacha tabia yake ya uhuni hata baada ya kuoa aliendelea kutembea na mabinti mbalimbali. Alijivunia utanashati wake na pesa aliyokuwa akiitengeneza kutokana na mambo ya mitindo. Na kwa sababu kwenye kazi yake alikuwa akikutana na mabinti wengi wazuri ndipo alipojikuta akipata maambukizi ya gonjwa hatari la UKIMWI. Alipomuona Shida kwenye gari aliapa kuwa lazima ampate kimapenzi na pale Shida alipopata matatizo aliona ni nafasi pekee yake kuitumia vizur

" Ila huyu demu ni mkali sana,anawazidi hata wale madem zangu wengine" aliwaza Baada ya Shida kujiandaa vizuri Kolumba alimbeba kwenye gari yake na kisha wakaelekea katikati ya mji kwa ajili ya kumfanyia Shoping Shida kwa sababu hakuwa na kitu chochote hasa mavazi Waliporudi nyumbani haikuhitaji kutongozana,tayali walikuwa wapenzi na mwisho wakajikuta wakishiliki pamoja. Penzi la Shida lilimfumba macho Kolumba sana,alijikuta akimpenda sana na mara nyingi walishinda pamoja.

" Itabidi huyu demu nimuhamishie Arusha kwenye tawi langu ili inshu zisijekumfikia wife nikashindwa kuendelea kufaidi uhondo Ndipo alipofanya utaratibu na kumuhamishia Shida kwenye tawi lake lililokuwa Arusha Na baada ya muda wakaanza mipango ya kufunga ndoa yao kisiri bila mke wake kujua.



Simu ya SHIDA kwa mchungaji

" Mchungaji mpaka hapo unajua nini kilichonitokea kanisani baada ya mke wa Kolumba kujitokeza kisha kusema wameshaathilika,sasa niambie au nioneshe kitu kinachoweza kunizuia kulipa kisasi?" akamaliza kusimulia Shida. Mchungaji hakuwa na usemi tena juu ya lile

" Shida usiue kwanza nipe nafasi nifikilie cha kufanya" akajibu Shida alikata ile simu na kisha akaondoka na kuingia mitaani. Alizunguka na kufikia eneo lenye bar wanazofikia watu wazito sana. Aliagiza kinywaji na kutulia kwa muda ndipo mhudumu akamfata na kisha Shida akampeleleza kuhusu Alex kwa sababu alikuwa akifahamu kuwa alipenda kuja bar zile tangu kipindi kile wakiishi wote.

" Unamuulizia yule tajili kijana Alex?" akajibu mhudumu

" Ndiyo,nahisi atakuwa yeye" akasema Shida Yule mhudumu alimchukua na kumpeleka eneo walilokuwa wakikaa watu wa VIP na kumuonesha Alex Shida alipatwa na hasira kali sana alipokumbuka jinsi Alex alivyoyafanya maisha yake kuwa ya taabu na matatizo Alipeleleza mpaka kugundua gari aliyokuja nayo pale,kisha akamzubaisha mlinzi wa eneo lile na kukata breki za gari ile kisha akaacha ujumbe kwenye gari ile na kutokomea. Alex alipotoka na kupanda gari ili aondoke hakugundua chochote ila akiwa njian akiona karatasi ndogo kwenye gari akaichukua na kusoma

" Mwanamme mshenzi Alex,ulinitafuta ili kuniua lakini hukufanikiwa,sasa ni wakati wangu wa kulipa kisasi,nimekata breki za gari yako utakufa kifo kizuri sana! Ndimi Shida" Baada ya kusoma ujumbe ule Alex alishtuka mpaka pombe zote zikamuisha kichwani Alipojalibu kukanyaga breki ziligoma,alijikuta akipaniki na kushindwa kuiongoza gari vizuri. Kasi ya gari ikazidi kuongezeka na mwisho ikamsababishia ajali kubwa sana huku yeye akipoteza maisha pale pale. Shida aliendelea na upelelezi wake kuhusu baba yake mzazi Filbert mpaka alipokuja kufahamu kuwa aliajiliwa kama mkufunzi kwenye chuo kikuu cha Dodoma. Kitu kilichomvutia zaidi ni baada ya kupata taarifa kuwa anapenda sana dogo dogo Ikabidi Shida ajitengeneze vizuri na kisha kuanza mitego yake ili kumnasa baba yake mzazi huyo. Baada ya siku kadhaa mitego yake ilinasa baada ya kufanikiwa kupata namba ya simu ya baba yake yule kisha kumtongoza kwenye simu mpaka mzee wa watu akaingia kwenye msitari Walipanga kukutana Hotelin na Shida alitangulia pale kisha akachukua chumba na kumsubiri baba yake ambaye alifika muda mfupi baadae Shida alimpatia kinywaji chenye madawa ya kulevya na kisha baada ya kunywa akamweleza ukweli yeye ni nani na anataka kumfanya nini? Yule mzee alijalibu kujitetea ila taratibu nguvu zikamuishia na Shida akamchoma visu mwilini mpaka alipohakikisha kuwa amefariki ndipo akatoroka. Upande wa Mchungaji alikuwa ameshatoa ripoti polisi na uchunguzi ukawa umeshaanza,taarifa ya vile vifo viwili iliwafikia polisi wakiwa kwenye uchunguzi. Shida baada ya kuwaua wale wawili alimlenga Kolumba kwa sababu ya kumwambukiza UKIMWI Alirudi Dar ghafla na kumpigia simu mchungaji kisha akamtaarifu kuwa ameshakamilisha kazi kwa watu wawili na bado mmoja na moja kwa moja mchungaji akajua atakuwa Kolumba,hivyo akawataarifu Polisi ambao walianza kufatilia Polisi walipofanikiwa kumpata Kolumba walikuta tayari ameshakuwa maiti na kila walipotafuta chochote cha kuwasaidia kumkamata mhusika hawakupata kitu. Taarifa ilikuwa kuwafikia Polisi juu ya mdada aliyekutwa huko Kiluvya akiwa kajinyonga nao wakaelea eneo la tukio. Pembeni yake kukiwa na ujumbe alioandika huku akielezea historia yake yote ya maisha na kilichosababisha afanye yale mauaji. Baada ya askari wale kuusoma ujumbe ule wakisikitika sana

" Kweli inatudbidi tuchague majina ya kuwaita watoto wetu! Jina ndilo lililomtesa binti huyu" aliongea askari mmoja

" Kweli kabisa" akajibu mwenzake Walichukua mwili ule kisha mchungaji akataarifiwa na kuja kuhudhulia mazishi yaliyofanya na serikali.

" Kwa jina la baba na la mwana na roho mtakatifu! Mungu iweke roho ya mwanao Shida mahali pema peponi, ameen" alimaliza mchungaji



**********


HATIMA.



KALAMU YA JUNIOR Kila tunachokifanya huwa kinaenda na mkono wa Mungu,hata majina tunayowaita watoto wetu yanawekewa mkono na baba Mungu,kuwa mwangalifu katika kumchagulia mwanao jina ili usijekuwa unamletea matatizo bali liwe la kumletea baraka.



MWISHO



Ahsante sana kwa kuwa pamoja name kuanzia sehemu ya kwanza mpaka ya mwisho. Hakika mmenijaza nguvu sana katika kazi hii. Nawashukuruni Sana.



Powered by Blogger.