KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Simulizi : Shida Sehemu Ya Kumi na saba (17)

Hadithi nzuri ya kusisimua ya shida
Shida alishikwa na uoga mkubwa baada ya kusikia akina Ally wakimuulizia kule sebuleni huku wakimtesa yule mhindi. Alijua muda wowote wanaweza kuoneshwa alipo hivyo akajalibu bahati yake ya misho. Alitoka kimya kimya kwenye kile chumba na kuingia kwenye kolido ili atafte njia ya kutoka. Kwenye kolido alimuona mzee mmoja mpishi na yeye akiingia kwenye chumba kimojawapo ikabidi amfate. Alipomfikia akakuta yule mzee anatoa mifuko kwenye eneo moja la ukutwa wa nyumba ile

"Tafadhali, nisaidie,hawa watu wananitafuta mimi pia,wataniua,nisaidie nitoloke kutoka humu nitaku a chochote utakachotaka" aliongea Shida Yule mzee aligeuka na kumwangalia kwa muda kisha akamwambia

" Nifate,hii njia ndiyo tunatumia kutolosha vitu kutoka humu kwa siri bosi asijue" Shida alimfata kimya kimya bila kuongea chochote kile na yule mzee alitoa ile mifuko mpaka tundu likaonekana. Wote wakapita kwenye lile tundu mpaka nje,yule mzee akaelekea kwenye kajumba kadogo kalikooonekana pale nje kama ni sehemu yao ya kupumzika huku Shida akimfata kwa nyuma. Waliingia ndani ya kile chumba na yule mzee akafunga milango

" Ahsante sana na Mungu atakulipia" akasema Shida

" Wala sihitaji huyo Mungu wako anilipe,umesema utanipa chochote kile nikikusaidia,sasa nahitaji penzi lako tofauti na hivyo napiga kelele kuwa uko hapa" akasema yule mzee

" Jaman hata huna huruma mzee wangu? Angalia mazingira tuliyopo kwa sasa" alijalibu kujitetea Shida Ila yule mzee hakumsikiliza,alianza kumvua nguo kwa nguvu Shida alijitahidi kupambana naye ila akawa anazidiwa nguvu Yule mzee alifanikiwa kumvua nguo zake za ndani,na yeye akanyenyuka ili avue za kwake na hapo hapo ndipo Shida akaona stuli iliyokuwepo pale pembeni akaibeba na kumpiga nayo yule mzee kwa nguvu zake zote kichwani mpaka akaanguka chini na kubaki kimya. Shida alichukua nguo zake na kuvaa haraka kisha akaanza kumsachi yule mzee,hakumkuta na kitu,akashachi kila sehemu pale ndani na bado hakupata cha maana,alipoangalia nguo yake ikawa na damu ikabidi aibe koti la yule mzee na kuvaa Alisubiri mpaka aliposikia milio ya risasi kisha miungurumo ya gari ikasikika pia

" Nina ile milion tatu niliyopewa na huyu mhindi,itanisaidia,napaswa kuelekea Dar es salaam niwe mbali na haya majanga" aliwaza Pale pale akaanza kunyata huku giza likimsaidia na kufanikiwa kutoka nje ya ile ngome ya yule mhindi. Huko nje alitembea mpaka akaipata njia ya lami na kuanza kuifata taratibu akiongeza kasi ya kutembea. Saa kumi na mbili ilimkuta stand ya mabasi . Akatulia sehemu akiangalia usalama wake eneo lile,alipohakikisha kuna usalama wa kutosha alielekea kwenye eneo wanalokatia tiketi na akatoa lile burungutu lake la pesa akalipita pesa ya tiketi kisha akarudisha zingine kwenye mfuko wa lile koti Alipotoka pale alielekea kwenye mgahawa mmoja akapewa chai na kunywa. Saa tatu gari za kuelekea Dar zilifika na yeye akaelekea gari ya Mohamed ilipokuwa akaanza kupambana ili kupanda. Nafasi pekee vibaka waliyokuwa wakiisubiria ili watimize walichopanga. Alipanda kwenye basi ya kutafuta namba ya siti yake akaiona na pembeni yake alikuwepo mkaka mmoja aliyevaa kinadhifu sana.



* * *

Kukutana na Mr Kolumba

" Samahani hiyo uliyokalia ni siti yangu " Shida alimwambia

" Bila samahani dada,ila kawaida ya watanzania tunaanza kwa salaam" akajibu yule mkaka. " Ooh! Samahani,habari yako?" akasalimia Shida

" Ni nzuri,kalibu kwenye siti yko" akasema yule mkaka akimpisha Shida kwenye ile siti ya dirishani. Shida akakaa na kutulia baada ya muda kidogo basi ikaondoka " Naitwa Kolumba sijui mwenzangu unaitwa nani?" akasema yule kijana " Naitwa Shida" akajibu kimkato Shida Kolumba alimwangalia kwa muda Shida kwenye nafsi yake akakubali kuwa yule binti ni mrembo na anayeweza kumfaa kwenye kazi yake.

" Samahani,naomba tufahamiane,mimi ni mwenyeji wa Dar es salaam,natoka Mwanza kwenye maonesho ya urembo,nina miliki kampuni ya urembo Dar,sijui mwenzangu" akasema Kolumba Shida hakumjibu bali alimwangalia tu bila kusema kitu. Kolumba alimuona kama binti anayelinga sana hivyo akaachana naye. Kolumba alitoa Ipod yake kisha akaanza kuchat na watu Facebook huku akiuplod picha za jinsi onesho lilivyoenda. Baada ya muda mfupi Shida alipitiwa na usingizi kwa sababu ya kutolala jana yake usiku hapo ndipo Kolumba akapata nafasi ya kumfotoa picha kadhaa. Basi ilisimama Dodoma kwa ajili ya chakula cha mchana na ndipo Shida alipoamka na kutaka na yeye anunue vitu. Alipoingiza mkono mfukoni kutafuta pesa yake hakuambulia kitu Alijitahidi kutafuta kila mfuko ila hakuona kitu,akaanza kukung'uta kila mfuko hakuambulia chochote

Shida hakuamini macho yake kuwa kapoteza kiwango kikubwa cha pesa vile,aliendelea kujisachi kila sehemu bila kuambulia kitu " Samahani dada,naona unajikagua tu kwa muda sasa ila sijajua una nn? Niambie yawezekana nikakusaidia" akasema Kolumba " Aaaah! Kakangu nahisi nimeibiwa,nilikuwa na kias kikubwa cha pesa na niliziweka mfukoni ila kwa sasa sioni kitu" akajibu Shida

" Mara ya mwisho uliziangalia muda gani?" akauliza Kolumba

"Nilienda kulipa wakati nakata tiketi na baada ya hapo nilienda kunywa chai na ndo mara ya mwisho kuziona" akajibu Shida

" Huo muda wote unalipa ulikuwa unazitoa zote kwa pamoja au ulikuwa umezigawa makundi?" akauliza tena Kolumba

" Hapana zilikuwa pamoja kwenye burungutu na nilikuwa nazitoa zote" akajibu Shida " Basi umeibiwa na vibaka,wakati unazitoa walikuona na kukufatilia utakuwa umeibiwa wakati unapanda basi kwenye ule msongamano" akasema Kolumba Shida alijiinamia pale kisha machozi yakafata kwa wingi kumiminika kwenye mashavu yake Kolumba alijitahidi kumbembeleza ila haikusaidia japo kidogo kwani Shida alikuwa katika wakati mgumu sana. Kolumba alitoka nje na kwenda kununua chakula cha kufunga chipsi na soda kisha akarudi na kumkabidhi Shida

" Ahsante kaka ila niko sawa" akajibu Shida

" Sikia,wewe ni mtu mzima,uache utoto wakati wa kulinga umeshaisha sasa unapaswa kuishi kulingana na nyakati,naomba ule hicho chakula kisha tujadiliane ninavyoweza kukusaidia pale ninapoweza" akasema Kolumba Shida alichukua kile chakula kwa aibu na kuanza kula mpaka alipomaliza " Ahsante sana kaka na ubalikiwe" akasema Shida baada ya kushiba

" Usijal nafikili ni wakati wa kufahamiana,unatokea wapi na unaenda kwa nani Dar?" akauliza Kolumba Shida akajikuta machozi yakianza kumbubujika kwa kasi,alijiuliza kama asema ukweli au afiche,ila mwisho akapa uamuzi

"Nina matatizo makubwa sana kakangu,sijui ninapotoka na sijui ninapoenda" akasema Shida

" Nieleze kila kitu bila kunificha ili nijue namna ya kukusaidia tafadhali" akasema Kolumba Ikambidi Shida aeleze kila kitu kuhusu maisha yake ya huko nyuma ingawa kuna vingine kama kufanya mauaji ilibidi afiche ili kuepuka kukamatwa na mkono wa sheria

" Pole sana dadangu,hayo ni ya Dunia,nitakusaidia kadri ya uwezo wangu pole sana" akasema Kolumba

" Ahsante sana kakangu nitashukuru zaidi ukinisaidia kwa sababu huko sina mwenyeji" akajibu Shida Njia nzima walikuwa na furaha wakipiga stor kwa pamoja na kusimuliana mambo mbali mbali huku Shida akiulizia mambo mbali mbali kuhusu Dar kwa sababu ulikuwa umepita muda tangu awepo kwa mara ya mwisho. Hatimaye usiku wa saa mbili waliingia Kibamba Dar es salaam



**********
INAENDELEA
Powered by Blogger.