KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Sitasahu sehemu ya Kumi (10)

hadithi nzuri ya kusisimua
Aliponikaribia niliyaona macho ya Tayana yakimaanisha kitu..macho ya upendo huku mdomo wake ukihitaji kusema kitu ni kama ameshikwa na kigugumizi....Tukasogeleana!...Tukatazamana!....Tukajikuta tunakumbatiana. Kumbatio lenye kufungua ukurasa mpya wa urafiki...nikapigwa na bumbuwazi...nikapoteza kumbukumbu nzuri na kuwaza ni lini hasa mara ya mwisho mimi kukumbatia ama kukumbatiwa na sio tu kukumbatiwa na binti, binti mrembo? 

Nilihisi mwili wangu umepigwa na shoti ya umeme...shoti iliyokuwa inasambaa mwilini kwa wakati huo....akili haikutaka..zaidi ilikuwa uzoefu wenye kuvutia sana. " Nakupenda Richard, nakupenda sana Richard natamani uwe mume wangu Richard hata sasa" Alinitamkia Tayana bila woga. Nikashtuka!.... Nikavutwa! nikavutika! kizuri hapa ni kwamba tayari mimi nilishapenda tangu siku ya kwanza nilipomuona. Nikamjibu nampenda pia .....Tukaachiana.....

Tayana akaniita.."Richard? Nataka kukukabidhi moyo wangu, tangu sasa nakukabidhi moyo wangu siwezi kuendelea kuumiza moyo wangu...sitaki kuhisi nakupenda...nataka kukwambia nakupenda Richard. Hichi nilichokuwa nacho kitakuwa kwa ajili yako peke yako, naapa sitampa mwingine sitakuumiza na naomba husiniumize Richard..tazama ujasiri niliouonesha Richard kwako?....Ni wanawake wachache wenye ujasiri kama wangu wa kumtamkia mwanaume hisia zake..tafadhali kubali ombi langu Richard...Husinikatili Richard, mimi ni kiumbe dhaifu mbele yako Richard."

Nilimtazama Tayana kwa mshangao...nilivutiwa na ujasiri wake....bila kuchelewa nilimjibu...'Too late Tayana'...Nikamuona Tayana akishangaa! uso ukapoteza tabasamu lililokuwepo...nikagundua!.."sivyo ufikiriavyo Tayana" Nilimueleza.....akabakia ameshikwa na mshangao wenye taharuki! ... Nilikupenda tangu siku ya kwanza nilipokutia machoni Tayana. 

Nilipokuona siku ile kwa mara ya kwanza mwili wangu ulinisisimka na nikajua huyu ndiye mwanamke niliyekuwa namsubiria. Mwanamke wa ndoto yangu. Hata hivyo siku ile nilifikiri kama jambo hilo lisingewezekana milele...tofauti yangu na yako ilikuwa kubwa. Nikasahau mapenzi yana mambo mengi...mapenzi ni kama sanaa ambayo unaweza kuyatengeneza ukiamua karibu ndani yangu Tayana.....Sitakuumiza..nitakulinda Tayana. I don't know what happened........Hakika Tayana alivutiwa na mapishi yangu niliyomuandalia siku hiyo...

==============================================================
Miezi sita baadaye mkono wangu wa kiume ulikuwa umemshika Tayana pembeni yangu ndani ya kanisa ya St Joseph tukielekea kwenye antare kwa ajili ya kiapo cha ndoa....ndani ya kanisa hilo lililojaa pomoni....furaha ilinitawala kila nilipowaona wazazi wangu wakifurahia......nawatazama marafiki wakinishangilia...najikuta nikiamini mimi ndiye mwanaume mwenye furaha kuliko wote Duniani. Tayari ninaye mkononi mwangu mwanamke mrembo anayeenda kutimiza ndoto zangu. Ndoto ya kuwa na mke mzuri....mke mrembo mwenye kujivunia kwa marafiki. 

Baada ya kula kiapo nikamgeukia Tayana ambaye sasa ni mke wangu rasmi nikamwambia; " Uwepo wa mmoja haukamiliki mpaka uwepo wa mwenza..asante moyo..asante moyo kwa kupenda" Mwanamke aliyenipatia Mungu.
Mwisho wa Richard....Twende kwa Tayana naye tumsikilize kwa ufupi...ana lipi ambalo anahitaji jamii ijifunze kupitia yeye

INAENDELEA

Powered by Blogger.